Na wandishi Wetu
MABONDIA Baina Mazola 'Simba Mazola' na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' wamendelea kutambiana kwa ajili ya mpambano wao ujao utakaofanyika Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mpambano wa raundi nane uzito wa kg 57
Wakiongea kwa nyakati tofauti kambi hizo zimejimba kila mmoja kumpiga mwenzake raundi za awali
Kwa upande wa Miyeyusho amejigamba kuwa katika mabondia wa Mabibo wanaofundishwa na kocha Cristopher Mzazi akuna anae msumbua ata mmoja hii ni pambano la kisasi ukumbuke kuwa Mzazi ana mabondia wengi na mimi ndie ninae mwalibia mara ya kwanza nilimvunja mbavu bondia wake Ramadhani Shauli akakaa mbali na mchezo wa ngumi mwaka mzima wakaniletea bondia mwingine Nassibu Ramadhani nae nikafanya hivyo hivyo sasa wamemleta huyu Mazola nita akikisha navunja mbavu kama nilivyo wafanyia wenzake wawili
Kwa upande wa Mazola nae ametamba kumsambalatisha mpinzani wake raundi za mwanzo kwani ana jipya ukumbuke mchezo wa ngumi sio sawa na michezo mingine umri ukienda biashara imekwisha sasa naenda kumstafisha ngumi rasmi yule babu hivyo wapenzi waje kwa wingi siku hiyo ili waone ninavyo mwachisha ngumi.
Nae mratibu wa mpambano huo kaizirege Dragon Kaizum amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakati bondia kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' atakumbana na Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashidi Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani
Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.