KIKAO Cha baraza maalum la madiwani kilichokaa Tarehe 21/8/2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kimeahirishwa baada ya waheshimiwa madiwani kugoma kuendelea na kikao hicho, wakilalamikia kutopewa makabrasha kwa wakati kwa mujibu wa kanuni za vikao na kutokuwepo kwa CAG.
Wakiwasilisha
hoja hiyo madiwani hao wamesema
kwa mujibu wa kanuni wanatakiwa kupata makabrasha hayo siku saba kabla ya kikao ili kuyapitia kifungu baada ya kifungu kwa umakini badala
yake wameyapata jana hivyo hawajayapitika kwa kuyasoma na kuongeza kuwa mkuu wa
wiliya alishaagiza wapatiwe makablasha hayo kwa kufuata utaratibu.
Akizungumzia
sababu ya kucheleweshwa kwa makabrasha hayo mkurugenzi wa halmashauri ya
Sengerema Bonifasi Mafuru Magesa amekili kosa hilo na kusema kuwa ni kutokana na ratiba ya uzinduzi wa Mradi mkubwa wa maji ambao ulikuwa na ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli na
Mwenge wa Uhuru ndiyo chanzo cha kutokupata makabrasha kwa wakati.BOFYA HAPA KUSIKIA KILICHOJIRI
Kwa upande wake
mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngereja
ameshauri kuahirishwa kwa kikao hicho kutoka na na mapungufu yaliojitokeza ili
kukidhi vigezo.
Naye mkuu
wa wilaya ya Sengerema Mhe. Emmanuel Kipole amesekitisha na ofisi ya mkurugenzi
kwa kutokufuata utaratibu na maagizo ambayo aliyatoka katika balaza lililopita
kwa kumtaka mkurugenzi kuhakikisha makablasha yanapatikana kwa wakati.
Akiahirisha
kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya wa Sengerema ambaye pia ni
diwani wa kata ya Nyamatongo Mhe. Evarist
Yanga ameunga mkono maamuzi ya waheshimiwa madiwani na kuahirisha
kikao hicho hadi tarehe 23/8/2017
KIKAO HICHO
KILICHOKUWA NA DHUMUNI LA KUPITIA NA KUJADILI TAARIFA ZA MKAGUZI WA HESABU ZA
SERIKALI (CAG) KIMEAHIRISHWA HADI KESHO ALHAMISI YA TAREHE 24/8/2017 SAA TATU ASUBUHI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.