Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Botswana utakao pigwa Septemba 2 mwaka huu.
Wachezaji hao wa Taifa Stars wanatarajia kuingia kambini Agosti 27 siku ya Jumapili saa mbili usiku nakuanza mazoezi tarehe 28 ya mwezi huu tayari kwa maandalizi ya mchezo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema “Tunategemea kuanza kambi siku ya keshotarehe 27 saa mbili usiku hapa hapa Dar es salaam na tunategemea kuwa na vijana 21 kambini ambao watafanya mazoezi sikua ya Jumatatu jioni na kumaliza mazoezi tarehe 1 na siku inayofuata ndiyo mchezo wetu na Botswana katika uwanja wa Uhuru”, amesema Mayanga.
Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Alfred Lucas amesema “Kutakuwa na mabadiliko ya ratiba ya ligi kwa sababu tulitarajia zaidi kwamba tarehe za FIFA zisianze tarehe 28 tulitegemea zingeanza baadaye lakini wao wametuletea taarifa nafikiri ilikuwa wakati ule wa uchaguzi ambao kidogo wameturudisha nyuma tuliamini ingekuwa tarehe tano na kuendelea la kini wao wamerudisha tena nyuma”.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.