TUME ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa
nchini Kenya imetangaza kuwa, inachunguza makundi 21 ya Whatsapp
yanayosambaza ujumbe wa chuki na uchochezi kuelekea uchaguzi mkuu mwezi
ujao katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa tume hiyo Francis Ole Kaparo amesema kuwa, tayari
wameanza mchakato wa kuwahoji wamiliki wa makundi hayo ya Whatsapp
kutoka kaunti 21 nchini humo.Kaparo amesema kwamba, tume yake itawafungulia mashtaka wale wote wanaochochea au kutuma ujumbe wa chuki kwa lengo la kuzua machafuko kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe nane mwezi ujao. Serikali imetangaza kuwa, haitakubali watumiaji wa mitandao kuvuruga amani kwa kueneza habari za uzushi.
Wakenya wametakiwa kutumia vyema mitando ya kijamii na kujiepusha na uchochezi. |
Kwa upande wa vyombo vya usalama, inspekta jenerali wa polisi Joseph
Boinet amesema polisi watatumia nguvu kiasi kuwakabili wachochezi wa
ghasia iwapo fujo zitazuka. Onyo lake linakumbusha matukio ya mwaka
2007/08 wakati polisi walipotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kiholela
walipokuwa wakikabiliana na ghasia.
Huku hayo yakiripotiwa, wasiwasi umeendelea kutanda katika Kaunti ya Lamu kutokana na kuongezeka mashambulio ya wanamgambo wa kundi la al-Shabab katika siku za hivi karibuni. Sambamba na hayo, kampeni za uchaguzi zimeendelea kupambana moto huku vyama vikuu vya Jubilee na Muungano wa NASA vikiendelea kupiga debe la kuomba kura.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.