ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 4, 2017

RAIS JPM AZINDUA MRADI WA MAJI SENGEREMA, ASEMA ANA SIRI NZITO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli akihutubia wananchi wa wilayani Sengerema eneo la Chanzo cha maji Nyamazugo ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi na mausafi wa mazingira. Mradi huu umetekelezwa chini ya Mpango wa LVATSAN - ii na kusimamiwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza (MWAUWASA)
Jiwe la msingi la mradi wa maji Sengerema.
Naam ndivyo inavyosomeka katika mradi wa maji Sengerema.
Shekhe Kabeke.
Askofu wa Jimbo Katoliki.
"Utekelezaji wa Mradi kama huu umefanyika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, chini ya Ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika ABD ambapo katika nchi ya Tanzania unatekelezwa katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe, Sengerema na mkoani Geita". Katibu Mkuu Wizara Ya Maji na Umwagiliaji Kitila Mkumbo
Mbunge wa Sengerema John Ngeleja akimkaribisha Mhe. Rais Jimboni kwake.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa Dr. Charles Tzeba naye alipata fursa kuzungumza na kuwasilisha changamoto za watu wa jimbo lake kuhusu umeme na maji kwa Mhe. Rais Magufuli ambapo Serikali tayari imekwisha weka mpango mkakati ambao unafuatana na utekelezaji.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela mbele ya umma wa wananchi waliofurika wilayani Sengerema kwenye uzinduzi wa eneo la Chanzo cha maji Nyamazugo ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi na mausafi wa mazingira. Mradi huu umetekelezwa chini ya Mpango wa LVATSAN - ii na kusimamiwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza (MWAUWASA)
Sehemu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza (MWAUWASA) kwenye tukio wilayani Sengerema.
Mahala walipoketi viongozi wa Chama na wakuu wa ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza.
Kikundi hiki kilitia hamasa kubwa sana kwenye kusanyiko hilo.
Utu uzima dawa na kwenye kusanyiko hili wanakwaya hawa walifanya mambo makubwa kiasi cha kutia furaha na tabasamu kwa wahudhuliaji.
Wana Kekundu kutoka katika kanisa la AICT Makongoro Mwanza wakitumbuiza kusanyiko
la eneo la Chanzo cha maji Nyamazugo ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi na mausafi wa mazingira. Mradi huu umetekelezwa chini ya Mpango wa LVATSAN - ii na kusimamiwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza (MWAUWASA)
Kusanyikoni:- Kukamilika kwa mradi huu kumewatua ndoo kichwani akinamama waliokuwa wakilazimika kuamka alfajiri na kutembea umbali mrefu kusaka huduma ya maji safi na salama kwenye mabwawa, visimani na katika Ziwa Victoria.
Awali akimkaribisha Dr. John Magufuli kuzindua mradi huo, Waziri wa Maji na Umwailiaji Mhandisi Greyson Rwenge amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha inafikisha huduma za maji safi na salama katika mikoa yote navijiji vyote ili kutimiza malengo ya maisha bora.
Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika uchaguzi uliopita 2015 Hamisi Tabasamu ambaye ametambulishwa rasmi kurejea CCM na Mwenyekiti Anthon Diallo (kushoto aliye nyanyua dole guma) na Katibu wake (kulia) ameibua ufisadi mkubwa ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Sengerema wa Shilingi bilioni 2.4 za kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika uchaguzi uliopita 2015 Hamisi Tabasamu akisalimiana na Mhe. Rais Magufuli mara baada ya kupokewa rasmi ndani ya CCM.
Kusanyiko:-

AKIKAZIA KUHUSU SUALA LA MIMBA MASHULENI.
Rais Magufuli amesema mwalimu mkuu atakayeruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi shuleni kuendelea na masomo katika shule za Serikali, atafukuzwa kazi.
 
“Ni ukweli pia kuwa wanafunzi waliopata mimba hawarudishwi shuleni, kuna ujanja ujanja wa walimu, wanaandika cheti kuwa alikuwa amelazwa,” amesema na kuongeza:

“Nikimuona Headmaster, amerudisha mwanafunzi aliyepata mimba, kwenye shule za Serikali, yule mwalimu anaondoka.”

Rais amehoji: “Wote waliopata mimba wamebakwa?” Alihoji na kuendelea, “wanafanya mambo haya kwenye picha, wakipata mimba kwa namna hiyo arudi shule.”

Ameongeza: “Niwaombe wazazi wawachunge watoto, hizi mimba zinatokana na wazazi wetu ni lazima wazazi tujifunze kulea, tumechagua kueleza ukweli, tuambiane ukweli.”
Sura za uelewa na kutafakari ndani ya kusanyiko la uzinduzi mradi wa maji Sengerema.
Kusanyiko la uzinduzi.





Wandishi wa habari na maripota wa vituo mbalimbali wakipata picha na Mhe. Rais JPM sanjari na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
Eneo la Chanzo cha maji Nyamazugo ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma ya majisafi na mausafi wa mazingira. Mradi huu umetekelezwa chini ya Mpango wa LVATSAN - ii na kusimamiwa na Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza (MWAUWASA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.