Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, imesema kuwa mmoja wa
mameneja wake wa masuala ya teknolojia Chriss Msando, hajulikani aliko.
IEBC inasema kuwa Msando alionekana mara ya mwisho siku ya Ijumaa jioni.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa mtu huyo aliyafanya siku ya Jumamosi
mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS na mmoja wa
wafanyakazi wenzake.
Aliyoandika kwenye ujumbe huo yalionyesha kuwa alikuwa akijielewa na alikuwa na mipango ya siku.
Ripoti tayari imepelekwa kwa polisi huku IEBC, familia yake na pia polisi wakishirikiana kujaribu kubainia aliko.
Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.