Rais Magufuli baada ya kuwasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa 10 jioni, msafara wake ulipofika kona ya Bwiru wilayani Ilemela ulisimama na kisha kuanza kuzungumza na wananchi kwa takribani dakika 5 na kuondoka.
Rais John Magufuli, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la ndege, sanjari na wale wa Airport Mwanza.
Msafara ndani ya uwanja wa ndege wa Mwanza Mhe Rais akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
Rais John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
John Magufuli, salaam kwa wadau viwanjani hapo.
Viongozi balimbali wa vyama, serikali, dini na kada mbalimbali wakiwa katika mstari mmoja kwaajili ya mapokezi ya Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli,
Rais John Magufuli akisalimiana na kada wa Chama cha Mapinduzi.
Ngoma asili viwanjani hapa.
Msafara ulipofika katikati ya Jiji ulisimama ghafla na kisha Rais Magufuli akamwaga neema kwa mwananchi mmoja mchuuzi mdogomdogo wa karanga aliyekuwa karibu na uwanja wa Mpira wa miguu wa Nyamagana kwa kunua karanga za kuchemsha toka kwa mwanamama mmachinga kwa gharama ya Sh. 100,000/=
Suala hili limetafsiriwa na wengi kuwa ni mtaji kwa mama huyo.
"Ndugu zangu biashara inaanzia chini, hawa ni wajasiliamali ambao ni wafanyabiashara wakubwa wa baadae hivyo ni lazima tuwalinde" Rais alisema Rais Magufuli.
Na kisha kuongeza kwa msisitizo "Narudia hakuna mmachinga kusumbuliwa, uko mpango madhubuti, tutatoa vitambulisho kwa wamachinga wote ili wawe na uhuru wa kufanya biashara kwa kanuni siyo holela holela"
Rais Magufuli amesema ameamua kpambana na ufisadi ili kila mtanzania anufaike na Tanzania.
Baada ya hapo akaelekea moja kwa moja katika uwanja wa michezo wa Nyamagana kujionea maendeleo yake na jinsi ulipofikia akisisitiza kuwa uwanja huo una historia kubwa naye anajivuni kuwa mmoja wa watu walio upigania kutobadilishwa matumizi yake kwani kipindi cha nyuma matajiri wachache walitaka kujimilikisha na kujenga hoteli kubwa ya kisasa kwa kisingizio kwamba humo ndani kungekuwa viwanja vidogo vya michezo ya ndani.
Jeh Safari hii itakuwa na neema kwa wadau wa soka mkoa Mwanza kwa kiwanja hicho kupata majukwaa na kumaliziwa baadhi ya changamoto ambazo mpaka sasa hazijapata tabibu? Hilo ni swali la wananchi wengi.
Ndani ya uwanja wa Nyamagana kulikuwa na mchezo wa ligi daraja la nne uliokuwa ukiendelea kati ya Buhongwa na Nyamwaga, naaam Rais alitinga katikati ya uwanja ambako pia alisalimiana na timu zote mbili kisha akakagua uwanja, akacheki mchezo kwa dakika kadhaa na kisha kuondoka eneo hilo kuelekea ikulu ndogo ya Capripoint Jijini Mwanza tayari kuanza rasmi ziara yake hapo kesho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.