Michuano ya Nyamagana Draft Championship inafika tamati leo ambapo jumla ya timu 18 toka kata zote wilayani Nyamagana zimekutana ukumbi wa Ghand Hall hapa kuchuana.
Nyamagana Draft Championship ni mashindano ya mchezo wa draft yaliyoanzishwa takrinan miezi miwili iliyopita chini ya mwasisi wake Mbunge wa Jimbola Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula.
Yakishirikisha kata zote 18 kila kata zilikuwa zikishindana kuhakikisha zinapata timu moja yenye wachezaji wa 4 wa 4 watakaocheza fainali.
Leo tarehe 16 July 2017 ndiyo fainali yenyewe kusaka bingwa.
KAULI YA MBUNGE:-
Sote tunafahamu kuwa mchezo wa bao upo lakini hatujawahi kuufuatilia na kuutilia maanani kama michezo mingine ambayo hii leo twaiita mikubwa.
- Ukubwa wa mchezo unatokana na kuzingatiwa, kujengewa misingi na kupewa kipaumbele.
- Mchezo huu unahistoria kubwa sana kwa watanzania ni zao la mchezo wa bao ambao hutumia kete na mashimo.
Jimbo la Nyamagana limeamua kuufanya mchezo huu kuwa moja kati ya michezo ya kimashindano na hata kuufikisha ngazi ya mkoa, taifa na ikiwezekana kimataifa.
Mashindano yanakamilika leo nayo hamasa imekuwa kubwa sana wachezaji wamejitokeza ingawa mwanzo walidhani ni masihala hivi lakini leo katika hatua ya mwisho mchezo umekuwa mkubwa hata zile kata ambazo hazikushiriki mwanzo, kwa kasi leo wanatamani kuingia kwenye hatua hii na kuwa sehemu ya washiriki.
Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni shilingi laki 4, kikombe na medali ya dhahabu.
Nafasi ya pili na watatu medali.
Lengo ni kuu ni kutengeneza wigo wa kuwa na michezo mingi na kutoa fursa kwa wenye uwezo na michezo hiyo ikiwa ni sambamba na kujenga urafiki, udugu, ushirika na kufahamiana.
"Wengi kutokana na ubize na harakati za maendeleo hatupati muda wa kukutana pamoja kutengeneza ushirika hivyo leo tunakutana hapa wadau wa kata 18 si kitu cha kawaida" Kisha akaongeza
"Kuna watu zaidi ya 100 hapa watu hawa wanakutana kwa mara ya kwanza kwa sababu walikuwa hawana sehemu ya kukutana, katika kukutana huko watu watabadilisha mawasiliano, mwenye hitaji mmoja anakutana na mwingine ambaye ni mtoa huduma na mwenye huduma atakutana na msajili wa watoa huduma hivyo tayari jamii itakuwa imerahisisha jambo hapo la kiaendeleo hata bila ya kutumia nguvu"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.