Jumla ya Tsh 450,000
zimetolewa na Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA mkoa wa Njombe Lucia Mlowe ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi
unaoendelea katika shule ya msingi Kambarage.
Hatua hiyo imekuja
ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mbunge huyo mwezi machi mwaka huu
katika harakati za kuhamasisha ujenzi wa shule ya msingi kambarage iliyopo
katika halmashauri ya mji wa Njombe.
Taarifa NA:AMIRI
KILAGALILA
Akimwakilisha mbunge
Lucia Mlowe, katibu wa mbunge huyo Bw.Semeni Deusi Msigwa amesema kiasi hicho
cha fedha ni kwaajili ya kuchangia mifuko ya saruji 26 pamoja na milango miwili katika kufanikisha
ujenzi unaoendelea shuleni hapo.
CUE….SEMENI MSIGWA
Pamoja na kutoa
shukrani mkuu wa shule ya msingi
Kambarega Jeni Resmu ng’umbi amewataka
viongozi wengine kuendelea kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.
CUE…JENI NG’UMBI
Kwa upande wake
mtendaji wa mtaa wa Kambarage Bw,izack mwakyusa pamoja na mambo mengine amesema
mchango huwa dira ya kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo katika mtaa huo.
CUE…. IZACK MWAKYUSA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.