Jeshi la nchi hiyo limetangaza
kuwa, waasi 12 wa Maimai na mwanajeshi mmoja wa serikali wameuawa katika
mapigano yaliyotokea jana baina ya pande hizo mbili kwenye eneo la
Kabasha la kusini mashariki mwa mji wa Beni wa Kivu Kaskazini.
Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kuwa,
waasi wa Maimai walishambulia eneo la Kabasha katika barabara ya
Beni-Butembo na kuwalazimisha wanajeshi kujibu mshambulizi hayo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi
baina ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa Maimai
katika eneo la Kabasha yalianza tangu siku ya Jumatano.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Asasi za kijamii za nchi hiyo zimesema kuwa, takriban wakazi wote wa eneo la Kabasha wamekimbia makazi yao.
Wakati huo huo jana Umoja wa Mataifa
ulitangaza kuwa, una wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea hali ya
vurugu na machafuko huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa katika masuala ya kusimamia amani baada ya kukamilisha
safari yake ya siku tano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Jean-Pierre Lacroix amesema kuwa,
vitendo vya kutumia mabavu na kuweko ripoti za ukiukaji wa haki za
binadamu katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo ni mambo ambayo yanatia
wasiwasi mkubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.