Jamii
imetakiwa kujifunza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kutokomeza vitendo
vya ukatili dhidi ya watoto ili kuhakikisha haki za watoto zinalindwa.
Wito huo
umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishana wa Polisi Ahmed
Msangi katika maadhimisho ya mtoto wa afrika mkoani Mwz.
Kutengana
kwa wanandoa na ukatili dhidi ya watoto kunatajwa kuwa chanzo kikubwa cha
watoto kutoroka majumbani na hatimaye kushia mitaani na wengine kuathirika
kisaikolojia na hivyo kusababisha kushuka kwa taaluma.
Watoto
wanaokulia mtaani wanatajwa kuwa wathirika wakubwa wa vitendo vya kikatili
ikiwemo ubakaji na ulawiti. Mwenyekiti wa madereva kanda ya ziwa DEDE PETRO ni
miongoni mwa watu waliokulia katika mazingira ya mtaani.
Jeshi la
polisi limewataka wananchi kutumia madawati ya jinsia yaliyopo kwenye vituo vya polisi kukomesha vitendo vya
kikatili dhidi ya watoto.
Utumikishaji
watoto, Mimba za utotoni,ubakaji na ulawiti kwa watoto imeelezwa kuwa miongoni
mwa changamoto zinazoikabili jamii kutokana na kutotoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na
wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.