Mjadala mkali umeibuka kati ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya pamba Tanzania Michael Mutunga kuhusu bei elekezi ya shilingi 1100 iliyokuwa imetangazwa na bodi hiyo,ambapo Mongella amesema serikali haiko tayari kujaribiwa na wanunuzi wa zao hilo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA MHE.MONGELLA
Mwenyekiti wa kikao cha kujadili maendeleo ya sekta ya pamba mkoani Mwanza John Mongella, pia ameagiza wakuu wa wilaya kuwakamata na kuwafungulia mashitaka wanunuzi watakaoenda kununua pamba bila utaratibu wa kupitishwa na halmashauri husika.
Sakata la kampuni ya Alliance iliyoingia mkataba na wakulima wa wilaya ya Magu, ambayo inadaiwa kushindwa kuwasaidia wakulima kwa kuwakopesha mbegu na madawa ya kuulia wadudu wanaoshambulia zao la pamba, limetawala mjadala huo baada ya mkuu wa mkoa kuagiza kampuni hiyo isiruhusiwe kununua pamba wilayani humo kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.