Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyo na Soko la hisa la Dar es salaam (Dar Es Salaam stock Exchange ) na kuanzia sasa itauza hisa zake kwa umma na kubadili jina lake kuwa Maxcom Africa PLC Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.