NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG,
Mkuu wa mkoa wa Mwz JOHN MONGELA amewapongeza raia wema
waliofanikisha kukamatwa na kuteketezwa kwa takriban ekari kumi za bangi ndani
ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja wialyani Sengerema Mkoani Mwanza.
MONGELA amesema wananchi wamepata hamasa ya kufichua maovu
katika jamii kutokana na imani waliyonayo kwa serikali ya awamu ya tano chini
ya rais JOHN POMBE MAGUFULI ambayo imekuwa ikifanyia kazi taarifa za siri
kutoka kwa raia wema.
Nchi imetangaza vita dhidi ya dawa za kulevya na makamanda
wa vita hivyo mkoani mwz wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo JOHN MONGELA
wamelazimika kutembea zaidi ya kilomita 20 ndani ya msitu wa hifadhi wa Buhindi
wilayani Sengerema wakisaka dawa za Kulevya, zikiwa ni siku chache tu tangu kisa
kama hicho kugundulika ktk msitu wa Maisome wilayani Sengerema.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwz AHMED MSANGI amesema uchunguzi
unaendelea kubaini wamiliki wa mashamba hayo ya bangi.
Misitu ya hifadhi imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya
uvamizi ambapo watu wamekuwa wakitumia misitu hiyo kama malisho ya mifugo,
kuchoma mkaa, kupasua kuni, mbao na mbaya zaidi kilimo cha bangi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.