Rais Magufuli ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya kuvunja Mamlaka hiyo Ikulu jijini Dar es salaam ambapo amehamishia majukumu ya Mamlaka hiyo katika Halmashauri ya Manispar ya Dododma ili kuondoa mkanganyiko kati ya vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.
Kufuatia uamuzi huo wa Dkt Magufuli pia ameivunja bodi ya CDA ambapo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Mhandisi Pascas Mlagila atapangiwa kazi nyingine naameagiza wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manisparya Dodoma na Ofisi nyingine za Serikalikadiri inavyofaa.
Aidha Rais Magufuli ameagiza hati za umiliki ardhi zilizokuwa zikitolewa na CDAkwa ukomo wa miaka 33 zibadilishwe na kufikia ukomo wa miaka99 kama ilivyo kwa maeneo mengine nchini ili kuwavutia wawekezaji hasa wa viwanda.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.