NA ALBERT GSENGO: ARUSHA
Mabingwa
wa Vodacom Premier League Dar es salaam Young African leo wameshusha
kichapo cha mabao ma 3-0 kwa timu ya AFC iliyo kuwa ikicheza nyumbani
kwake dimba la Sheik Amri Abeid mjini Arusha, katika mchezo wa kirafiki
wa kusherehekea ushindi na kulionesha kombe kwa mashabiki wake, baada ya
timu hiyo ya mtaa wa Jangwani mwishoni mwa juma lililopita kutawazwa
mabingwa wa VPL msimu wa 2016-2017 Tanzania Bara.
Wakicheza
mbele ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwa wingi mjini Arusha, Yanga
walifungua karamu yao kwa goli la kwanza lililofungwa na Jofrey
Mwashuiya kunako dakika ya 23, kisha baadaye mchezaji huyo huyo alirudi
kubisha hodi tena langoni mwa AFC na kufunguliwa kunako dakika ya 67 kipindi cha pili..
Samwel
Greyson aliyeingia badala ya Emmanuel Martin aliyeenda benchi aliizawadia Yanga bao la 3
na la ushindi ikiwa ni dakika 4 kabla ya filimbi ya mwisho ya mchezo kulia.
Mara baada ya mchezo Jembe Fm inazungumza na makocha wa timu zote mbili BOFYA PLAY KUMSIKILIZA MWAMBUSI.
Fikiri Elias ni mwalimu wa AFC ya Arusha naye alifunguka hivi:- BOFYA PLAY KUMSIKIA
Fikiri Elias ni mwalimu wa AFC ya Arusha naye alifunguka hivi:- BOFYA PLAY KUMSIKIA
Mashabiki dimbani Sheik Amri Abeid mjini Arusha AFC v/s Yanga.
Patashika ...
Zipo changamoto ambazo zinashabihiana na zile zinalo liandama soka la Mwanza.
Patashika ...
Zipo changamoto ambazo zinashabihiana na zile zinalo liandama soka la Mwanza.
Lakini jeh wajua nini sababu ya soka la Arusha kuporomoka? Mwakilishi
wetu Albert G Sengo alikuwa mjini humo naye hapa anazungumza na Kocha wa
zamani wa AFC, kwanza tahimini kisha nini sababu ya soka kuporomoka. BOFYA PLAY KUSIKIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.