ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 23, 2017

UTAFITI:- KARIBIA NUSU YA WAMAREKANI HAWANA IMANI NA SERIKALI YA TRUMP.


Utafiti mpya umeonyesha kuwa asilimia 42 ya wananchi wa Marekani wamepoteza imani na uongozi wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo katika kipindi cha siku 100 za kwanza ofisini.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na gazeti la Washington Post-ABC News, kiwango hicho kimevunja rekodi kwa kuwa ni cha chini sana na ambacho mara ya mwisho kilishuhudiwa nchini humo wakati wa utawala wa Dwight Eisenhower, rais wa 34 wa Marekani aliyeongoza kati ya mwaka 1953 na 1961.

Asilimia 58 ya Wamarekani waliohojiwa wanasema Trump hana ufahamu kuhusu changamoto na masuala nyeti ambayo wananchi wa nchi hiyo wanataka kuona yakitekelezwa na utawala wake.


Maandamano dhidi ya Trump nchini Marekani
Kadhalika asilimia 55 ya walioshirikishwa kwenye utafiti huo wa maoni wa Washington Post-ABC News wameeleza kutoridhishwa kwao na utendakazi na uendeshaji wa mambo wa serikali ya Trump.Wiki iliyopita, uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa na taasisi ya Gallop ulionyesha kuwa asilima 55 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa Rais Donald Trump hatekelezi ahadi zake alizotoa.

Hii ni katika hali ambayo, zaidi ya Wamarekani 40 elfu wakiwemo wasomi na wataalamu mashuhuri wa nchi hiyo wameshiriki kwenye maandamano mbele ya Ikulu ya Marekani White House, katika majengo ya Kongresi na Wizara ya Mazingira mjini Washington, kumpinga Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kulalamikia sera zake za mazingira.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.