ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 17, 2017

RIPOTI ZAIDI ZAVUJA KUHUSU URONGO WA MAREKANI JUU YA SHAMBULIZI DHIDI YA SYRIA


SIKU kumi baada ya shambulizi la makombora lililofanywa na Marekani dhidi ya kituo cha jeshi la anga la Syria cha Shayrat kwa kutumia kisingizio kwamba Damascus ndiyo iliyofanya mashambulizi ya silaha za kemikali katika eneo la Idlib, kumefichuliwa ripoti mpya zinazothibitisha urongo wa madai hayo ya serikali ya Washington.
Mtandao wa Anti-War umeripoti kuwa, afisa mmoja wa zamani wa serikali ya Marekani ameliambia jaraida la Truthout kwamba, masaa 24 kabla ya shambulio la Marekani dhidi ya kituo cha jeshi la anga la Syria, Warussia walikuwa tayari wameitaarifu serikali ya Washington kuhusu shambulizi lililokuwa limefanywa na jeshi la Syria dhidi ya ghala la silaha katika eneo la Khan Sheikhoun. 

Ripoti hiyo imetoa habari za kuaminika zinazoonesha kwamba, jeshi la Syria limeshambulia ghala la silaha za kemikali lililokuwa likijengwa na magaidi na kwamba Syria haikutumia silaha za kemikali katika shambulizi hilo. Hata hivyo Rais Donald Trump wa Marekani alitumia maudhui hiyo kama kisingizio cha kuhalalisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Syria kwa kisingizio kwamba imetumia silaha za mauaji ya halaiki.
Kituo cha jeshi la Anga la Syria kilichoshambulwia na Marekani, Shayrat
Jinsi Marekani ilivyolitumia kisiasa na kipropanda shambulizi lake dhidi ya kituo cha jeshi la anga la Syria kunaonesha kuwa, serikali za Washington na London zilikuwa na mpango wa muda mrefu wa kufanya mashambulizi ya kijeshi nchini Syria kwa shabaha ya kuyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kigaidi na kuiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo. 

Ripoti ya gazeti la Daily Telegraph la Uingereza imesema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo ataongoza mpango wa Uingereza na Marekani unaotaka kuyafukuza majeshi ya Russia nchini Syria na kumuwekea mashinikizo Rais Vladmir Putin wa Russia ili asitishe uungaji mkono wake kwa Rais Bashar Asad wa Syria. 

Vilevile Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson ameandika makala katika gazeti la Sunday Telegraph akisema, Moscow inapaswa kusitisha uungaji mkono wake kwa Rais Bashar Assad wa Syria na kujiunga na muungano wa Marekani na nchi za Magharibi huko Syria.

Mwaka 2003 pia Marekani ilitumia kisingizio cha kutaka kuharibu silaha za maangamizi ya halaiki kuishambulia na kivamia Iraq. Hata hivyo baada ya miaka kadhaa ya kuikalia kwa mabavu Iraq Marekani ilishindwa kuithitishia dunia madai ya kuwepo silaha za maangamizi ya umati nchini Iraq na ilishindwa kuonesha hata silaha moja tu ya aina hiyo. 

Wakati huo dunia nzima ilitambua kwamba silaha za maangamizi ya halaiki zilitumuwa tu kama kisingizio cha kuhalalisha mashambulizi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Iraq. 
Askari vamizi wa Marekani nchini Iraq
Hata hivyo Syria si Iraq. Ni miaka 6 sasa ambapo jeshi la Syria na wananchi wa nchi hiyo wamekuwa wakikabiliana kishujaa na makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa na kupewa misaada ya silaha na fedha na nchi za Magharibi na vibaraka wao kama Saudi Arabia, Uturuki na Qatar. 

Katika miezi kadha ya hivi karibuni jeshi la Syria limepata mafankio makubwa na kuyafukuza makundi ya kigaidi katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Mafanikio makubwa zaidi ya jeshi hilo hadi sasa ni kuwafukuzua magaidi wa Daesh katika mji wa Aleppo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Syria baada ya Damascus. 

Mafanikio hayo ya serikali ya Syria katika medani na viwanja vya vita yamekuwa na taathira kubwa pia katika medani za kisiasa na kuyaweka chini ya mashinikizo makubwa makundi ya upinzani ya washirika wao wa kigeni. 

Kwa msingi huo kambi hiyo iliyodhidi ya serikali ya Syria ilikuwa na haja ya kupata msukomo na matumaini mapya kwa ajili ya kuweza kukabiliana na kasi ya kusonga mbele kwa jeshi la Syria. Kwa mtazamo huo mashambulizi ya makombora ya Marekani dhidi ya kituo cha anga cha jeshi la Syria cha Shayrat yamewatia motisha na nguvu mpya magaidi walioko Syria. 


Jeshi la Syria likipambana na magaidi
Pamoja na hayo yote ni wazi kuwa serikali ya Syria, wananchi wa nchi hiyo na nchi zinazowaunga mkono hazitalegeza kamba hata kidogo mbele ya vitisho vya Marekani, waitifaki wake wa Ulaya na vibaraka wao kama Saudi Arabia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.