Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
amesema viongozi wanapaswa kuwasikiliza waandamanaji nchini humo ambao
wanamtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu au aondolewe madarakani baada ya
mabadiliko yake ya baraza la mawaziri kupelekea nchi hiyo kushushwa
kiwango cha kiuchumi.
Zuma
anatazamiwa kuachia ngazi kama mwenyekiti wa chama tawala cha ANC mwezi
Desemba lakini muhula wake wa pili wa urais utamalizika baada ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2019. Ramaphosa na mke wa wamani wa Zuma,
Nkosozana Dlamini-Zuma ni kati ya walio mstari wa mbele kuchukua nafasi
ya Zuma.
Inaaminika
kuwa Zuma anamuunga mkono mke wake wa zamani, huku Ramaphosa,
mfanyabiashara tajiri na mkuu wa zamani wa vyama vya kutetea haki za
wafanyakazi, akiwa na uungaji mkono miongoni wa waitifaki wa ANC katika
sekta ya leba.
Maandamano ya wananchi dhidi ya Rais Zuma wa Afrika Kusini
Matamshi ya Ramaphosa ni tafauti na ya Zuma ambaye anawatuhumu
waaandamanaji kuwa wana malengo ya ubaguzi wa rangi katika kumtaka
aondoke madarakani.
Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance na
vyama vingindgine vidogo vinaamini kuwa vinaweza kupata uungaji mkono
katika kumuondoa Zuma baada ya hatua yake tata ya kumfuta kazi Waziri wa
Fedha Pravin Gordhan aliyekuwa akiheshimika kitaifa na kimataifa.
Wakati huo
huo Zuma amesema hatajiuzulu huku akisema anapingwa kwa sababu
anazungumza haki. Akizungumza kanisani huko KwaZulu-Natal wakati wa
pasaka amesema wakati umefika kwa Waafrika wazalendo kufurahia matunda
ya uchumi.
Mahakama ya Katiba Afrika kusini inasikiliza kesi kuhusu iwapo kura
ya kutokuwa na imani na Zuma bungeni ifanyike wazi au kwa siri.
Wapinzani wanaamini kuwa iwapo muswada huo utafanyika kwa njia ya kura
ya siri utafanikiwa.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.