Kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Muda wa CUF bwana Julius Mtatiro
"Mwanasheria Mkuu wa chama chetu, Wakili Msomi HASHIM MZIRAY yuko katika
kituo cha Polisi Magomeni ambako amemsindikiza Mwenyekiti wetu wa
Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Juma Mkumbi.
Mhe. Juma Mkumbi ndiye aliyevamiwa na Mungiki wa Lipumba, akiwa
anaongoza Mkutano na vyombo vya habari pale Vina Hotel. Polisi
walipofika wakamshauri arejee nyumbani akapumzike (ana diabetes) kisha
wakamshauri akaripoti kituoni jana kwa ajili ya ku LODGE malalamiko yake
rasmi ili yaunganishwe na malalamiko ya waandishi wa habari na viongozi
waandamizi waliovamiwa juzi.
Jana mhe. Mkumbi alishindwa kwenda kufungua kesi kwani hali yake ya afya
haikuwa nzuri na leo ndipo alipanga kwenda. Ikumbukwe pia simu za jana
za OCD na OCCID za kutaka kuwapatanisha na wale wavamizi.
MAAJABU YA DUNIA...
Leo amekwenda Magomeni Polisi ili kuripoti tukio zima lilivyokuwa (kwani
Juzi Polisi walichukua maelezo ya wanahabari na viongozi waandamizi tu
wale waliokuwa wamepigwa, kuumizwa au kujeruhiwa).
Mkumbi amefika Magomeni Polisi ili kufungua mashtaka yake kama
muathiriwa lakini OCD na OCCID wa Magomeni wameelekeza ahojiwe kama
Mtuhumiwa. Hivi tuzungumzavyo Juma Mkumbi ndiye anahojiwa kwa tuhuma za
kumjeruhi yule MUNGIKI aliyekatwa mguuni na Wananchi (Mlinzi wa
Lipumba).
MAELEKEZO WALIYOPEWA POLISI..
Niliwaeleza hapa, kwamba Polisi wameelekezwa wahakikishe aidha upande
ULIOVAMIWA (Chama) unakubali kukaa meza moja na wale WALIOVAMIA (Lipumba
na Mungiki) AU Upande wa chama ndiyo unapewa kesi ya kujeruhi lile
jambazi lililojeruhiwa na wananchi.
HURUMA INAPONZA
Wananchi wenye hasira walipokuwa wanaliadhibu "ZOMBI" lile, liliokolewa
na viongozi wale wale walioshuka haraka chini na kuomba waitwe polisi.
Yaani, kama si juhudi za kina Juma Mkumbi na wenzao, zombi la Lipumba
lingeliuawa. Huruma yao kuingilia kati na kulikokoa na wakaita polisi
likakamatwa, ndiko kumewaponza. Polisi wanatufundisha kuwa the next
person wa Lipumba ambaye atatuvamia basi viobgozi waache auawe maana
wakimsaidia wao wanageuziwa kibao. Sawa tumeelewa somo!
BASTOLA
Hadi sasa, polisi hawaelezi lile ZOMBI lililokuwa na Bastola liko wapi
na hawasemi ile bastola iko wapi pia. Kwa kifupi Polisi hawataki
kuzungumzia masuala ya Bastola ile. Badala ya kushughulikia mambo
makubwa, sasa wana-deal na upande wetu.
WITO
Natoa wito kwa wanachama wa CUF kukaa STANDBY, tunataka kuona Zombi/Mungiki lililokamatwa na wananchi linafikishwa mahakamani.
Tunataka kuona wale wote waliokuwa na Zombi hilo wanakamatwa pia na
kufikishwa mahakamani. Wanafahamika kwa majina, kwa sura na kwa makazi.
Tunataka kuona ile BASTOLA inasakwa na aliyekuwa nayo anapatikana. Uzuri
aliyekuwa na bastola alipanda kwenye yale magari mawili yaliyotumika
kwenye uvamizi.
Tunataka kuona magari yaliyotumika kwenye uvamizi ule yakikamatwa NA madereva wa magari yale (wanafahamika) wanakamatwa haraka.
Tunataka kuona mkuu wa wavamizi wale anakamatwa haraka na jana
alionekana AZAM TV akitamba kuwa mazombi yake yataendelea na oparesheni
ya kuvamia na kupiga watu, (na polisi wana clips zote).
Kwa sababu leo tumekutana na Kamishna Sirro tunajipa muda kuona hatua
zipi zitachukuliwa. Kama hatua hazichukuliwi na Polisi, basi, sisi
tutawaambia wanachama wetu WASIFE KIKONDOO huko mitaani, tutawaomba
wajilinde kwa nguvu zote kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba. Kile
kijikundi cha MUNGIKI na LIPUMBA kina watu wachache sana, lakini UJINGA
wetu ni kuendelea kuheshimu sheria za nchi.
Mtatiro J,
24 April 2017."
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.