Burundi inaelekea kuathiriwa tena na mgogoro
wa kisiasa licha kufanyika juhudi za kikanda na kimataifa za kuupatia
ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, mgogoro wa kisiasa Burundi
ambao ulianza kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo wa
kusalia madarakani kwa muhula wa tatu mfululizo, umesababisha vifo vya
watu elfu mbili, mamia ya wengine kutoweka na maelfu kuwa wakimbizi
katika nchi jirani.Wakimbizi wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao. |
Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Tanzania ambaye ni msuluhishi katika
mgogoro wa kisiasa wa Burundi, ameshindwa kuandaa mazingira ya kufanyika
mazungumzo kati ya serikali na wapinzani licha ya kupita miezi kadhaa
hadi sasa, huku mashinikizo ya kimataifa kwa serikali ya Burundi
yakisalia bila kuzaa matunda.
Leo Jumanne tarehe 25 Aprili ni siku ya kukumbuka kutumia mwaka wa pili tangu kuanza mgogoro wa kisiasa huko Burundi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.