Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi. |
TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA
HABARI LEO TAREHE 06.03.2017
·
WATU
TISA (09) WAMEJERUHIWA KATIKA VURUGU WAKATI WA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA
WADOGOWADOGO SEHEMU ZISIZO RUHUSIWA WILAYANI NYAMAGANA.
KWAMBA
TAREHE 05.03.2017 MAJIRA YA SAA15:45HRS KATIKA MTAA WA BUHONGWA CENTER WILAYA
YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU TISA AMBAPO ASKARI MGAMBO WA JIJI LA MWANZA SABA (07),
AFISA MAZINGIRA MMOJA (01) NA DEREVA WA JIJI MMOJA (01) WALIJERUHIWA KWA KUPIGWA
NA MAWE SEHEMU MBALIMBALI MIILI YAO NA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO WALIOKUWA
WAKIFANYA BIASHARA PEMBENI YA BARABARA WAKISHIRIKIANA NA WATU WENGINE WALIOKUA
WAKISHABIKIA WAKATI WAKIENDELEA NA ZOEZI LA KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA
WADOGOWADOGO KATIKA MAENEO YASIYO RUHUSIWA HASWA KWENYE HIFADHI YA BARABARA YA
MWANZA KWENDA SHINYANGA.
MGAMBO
WALIOJERUHIWA NI 1. NDAISABAS NICODEMU
MIAKA 25, MKAZI WA MKUYUNI, AMBAYE AMEJERUHIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA
MWILI WAKE NA HALI YAKE BADO SIO NZURI, 2. ALEX JOSEPH MIAKA 25, MKAZI WA
ISAMILO, AMBAYE AMEVUNJIKA MGUU WA KULIA KWENYE PAJA, 3.EMMANUEL BIGAMBO MIAKA
37, MKAZI WA PASIANSI, AMBAYE AMEUMIA KIUNO, 4.ASIFIWE ANDREA MIAKA 33, MKAZI
WA IGOGO , AMBAYE AMEUMIA GOTI MGUU WA KULIA, 5. DAVID BAKARI MIAKA 32, MKAZI
WA NYAMANORO, AMBAYE AMEUMIA MGUU WA KULIA KWENYE GOTI, 6.ZACHARIA ANDREA MAIAK
24, MKAZI WA MKOLANI, AMBAYE AMEUMIA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NA KIDOLE GUMBA
CHA MKONO WA KUSHOTO NA 7.SURUSI JOSEPH MIAKA 21, MKAZI WA KILOLELI AMBAYE
AMEUMIA KIWIKO CHA MKONO WA KUSHOTO.
WENGINE
NI 8.FANUEL KASENENE MIAKA 39, AFISA MAZINGIRA WA JIJI LA MWANZA NA MKAZI WA NYEGEZI,
AMBAYE AMEJERUHIWA JUU YA JICHO LA KUSHOTO NA MDOMONI NA 9.GHARIBU AHAMADI
MIAKA 32, DEREVA WA JIJI NA MKAZI WA NYAKATO, AIDHA KATIKA VURUGU HIZO
KULIFANYIKA UHARIBIFU WA GARI LA HALMASHAURI LENYE NAMBA DFPA 2387 AINA YA SINO
AMBALO LILIVUNJWA VIOO.
AIDHA
WAKATI VURUGU HIZO ZINAENDELEA WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI AMBAPO ASKARI
WALIFIKA KWA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUDHIBITI VURUGU HIZO.
AIDHA KATIKA HARAKATI ZA KUDHIBITI VURUGU HIZO ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA
WATU TISA AMBAO INADAIWA KUWA WALIKUWA WAKIHUSIKA KATIKA VURUGU HIZO, JESHI LA
POLISI LINAENDELEA NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE TISA NA PINDI UCHUNGUZI
UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI WOTE WAPO HOSPITALI YA MKOA YA
SEKOU TOURE WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA
WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO AKIWATAKA KUTII SHERIA BILA SHURUTI ILI KUEPUSHA MAJERAHA
NA VURUGU ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANAWATAKA PIA WAFANYABIASHARA
WADOGOWADOGO KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BALI PINDI WANAPOKUWA
NA MALALAMIKO WATEUE VIONGOZI AMBAO
WATAPELEKA MALALAMIKO YAO KWA UONGOZI HUSIKA ILI YAWEZE KUTATULIWA KWA
AMANI.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.