SERIKALI ya Nigeria imetangaza kuwa, uwanja
wa ndege wa mji mkuu Abuja utafungwa kuanza leo Jumatano kwa muda wa
siku sita ili kupisha ukaratabati wa barabara za kukimbilia ndege.
Msemaji wa Wizara ya Anga ya
Nigeria amesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya mashirika kadhaa
ya ndege kusitisha kutua ndege zao katika uwanja huo.
Taarifa ya Wizara ya Anga ya Nigeria
imesema kuwa, sasa wasafiri wanaotumia uwanja huo watahamishiwa katika
uwanja wa ndege wa Kaduna uliopo yapata kilomita 160 kaskazini mwa mji
mkuu Abuja.
Wasafiri hao watasafirishwa kwa mabasi
na misafara yao kusindikizwa na askari wa kikosi cha ulinzi kutokana na
miaka ya hivi karibuni kushuhudiwa vitendo vya utekaji nyara katika njia
ya kuelekea Kaduna.
Barabara ya kukimbilia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Abuja. |
Serikali ya Nigeria imesema kuwa, inatumai mashirika ya ndege ya
kimataifa yatakubali kuutumia uwanja wa ndege wa Kaduna kama mbadala
hadi ukarabati wa uwanja wa Abuja utakapokamilika. Hata hivyo mashirika
kadhaa ya ndege ya kimataifa yakiwemo ya British Airways, Lufthansa na
la Afrika Kusini yametangaza kuwa hayatatumia uwanja wa ndege wa Kaduna.
Hadi sasa ni Shirika la Ndege la
Ethiopia tu la Ethiopian Airlines ndilo lililotangaza kuwa, liko tayari
kuutumia uwanja wa ndege wa Kaduna.
Baada ya kuweko habari za kugongana
kuhusiana na siku hasa ya kufungwa uwanja wa ndege wa Abuja, James
Odaudu msemaji wa Wizara ya Anga ya Nigeria amethibitisha kuwa, uwanja
huo utafungwa kuanzia leo Jumatano.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.