ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 21, 2017

SENETA FEISTEIN: KUNA UWEZEKANO MKUBWA DONALD TRUMP ATAJIUZULU MWENYEWE

SENETA wa chama cha Democrat nchini Marekani amefichua kwamba, kuna uwezekano mkubwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo atajiuzulu.

Vyombo vya habari vya Marekani vimemnukuu Seneta Dianne Feinstein ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti la Marekani kwa niaba ya watu wa Los Angeles akisema kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo atajiuzulu yeye mwenyewe kabla ya kulazimishwa kuachia ngazi.

Seneta Dianne Feinstein amesema kuwa, ana taarifa ambazo hawezi kuziweka wazi kwa sasa na kuongeza kuwa, Wamarekani wanataka kujua uhakika wa mambo. 

Amesema kuwa Trump amekuwa akikiuka sheria kila siku na kwamba anatarajia kwamba kiongozi huyo atajiuzulu kabla ya kulazimishwa kung'atuka madarakani. 

Seneta Dianne Feinstein

Matamshi hayo ya Seneta Dianne Feinstein yametolewa baada ya wananchi wa Los Angeles kuandamana wakiitaka Kongresi ya Marekani kuchukua hatua za dharura za kumuuzulu Donald Trump. Waandamanaji hao pia wanamtuhumu Rais huyo wa Marekani kwamba anakiuka sheria na katiba ya nchi.

Wakati huo huo miji mbalimbali ya Marekani imeendelea kukumbwa na maandamano ya maelfu ya raia wanaopinga sera na siasa zake hususan kuhusu masuala ya bima ya afya na wahajiri. 
Mpango mbadala wa bima ya afya wa Donald Trump uliopangwa kuchukua nafasi ya ule wa Obamacare wa rais aliyestafu, Barack Obama utawaathiri mamilioni ya Wamarekani na kuwafanya wapoteze bima zao za afya. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.