Gazeti la al-Wasat limeripoti
kuwa, Hassan Isa, mmoja wa viongozi wa chama cha Kiislamu cha al-Wefaq
amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, kwa tuhuma bandia za 'kufadhili
ugaidi'.
Mwanachuoni huyo ambaye pia alikuwa
Mbunge wa chama cha al-Wefaq anatuhumiwa kuhusika katika hujuma
iliyopelekea kuuawa maafisa wawili wa polisi na wengine kadhaa
kujeruhiwa, madai ambayo amekuwa akiyakanusha vikali.
Namna utawala wa Manama unavyotumia mkono wa chuma dhidi ya waandamanaji wasio na silaha nchini Bahrain
Namna utawala wa Manama unavyotumia mkono wa chuma dhidi ya waandamanaji wasio na silaha nchini Bahrain
Wakati huohuo, mahakama ya Bahrain
imewahukumu adhabu ya kifo Mohammed Ibrahim al-Tawq na Mohammed Radi
Abdullah, wanaharakati na wakosoaji wakubwa wa serikali wa
Manama. Kadhalika wanaharakati wengine watano wamehukumiwa adhabu ya
kifo, ambapo wanne kati yao wamepokonywa uraia.
Haya yanajiri wiki mbili baada ya
utawala wa wa ukoo wa Aal-Khalifa kuakhirisha tena kutolewa hukumu dhidi
ya Sheikh Isa Qassim, mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain hadi Mei 7 mwaka
huu.
Utawala wa kiukoo wa Bahrain unamtuhumu
Sheikh Qassim kwamba amekuwa akieneza chuki za kimadhehebu miongoni mwa
watu wa nchi hiyo, kuchochea machafuko na kuhatarisha usalama wa taifa.
Ikumbukwe kuwa nchi kadhaa za Kiarabu
hususan Saudi Arabia zimetuma wanajeshi wao nchini Bahrain kwa ajili ya
kuwakandamiza raia wanaoandamana kwa amani kupigania haki zao za
kimsingi kabisa kama vile haki ya kujichagulia wenyewe viongozi wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.