ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 6, 2017

AJIRA ZA KUDUMU KWA MADEREVA NCHINI ZITASAIDIA KUPUNGUZA AJALI BARABARANI.


NA ZEPHANIA MANDIA.


Waajiri nchini wametakiwa kutoa ajira za uhakika kwa Madereva badala ya kuwatumia kama vibarua, ili kupunguza tatizo la ajali za Barabarani zinazochangiwa na Madereva, kwa lengo la kuongeza kipato chao cha siku kupitia posho wanazopatiwa na waajiri..


Posho bila mshahara, ndicho kilio kinachotajwa kuwa chanzo kikubwa kinachochangia ajali za barabarani, ambapo watanzania wengi tayari wameshapoteza maisha kutokana na ajali hizo, zinazosababishwa na shinikizo la kipato duni wanachopatiwa Madereva na waajiri.


Akizungumza wakati wa kuwakabidhi Vyeti wahitimu wa kozi ya Udereva katika Chuo cha Mafunzo na ufundi stadi (Veta) mkoa wa Mwanza, Mratibu wa Kozi fupi na ujasiriamali wa Chuo hicho Peter Mlacha, amewashauri Madereva kutokukubali kuajiriwa kama vibarua. BOFYA PLAY KWA VIDEO HAPO JUU KWA TAARIFA ZAIDI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.