ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 28, 2017

WAVUVI HARAMU WATATU WANASWA WAKIWA NA KILO 500 ZA SAMAKI WALIOVULIWA KWA NJIA HARAMU ZIWA VICTORIA


Samaki wachanga wasio na viwango waliovuliwa ziwa Victoria mkoani Mwanza na kukamatwa.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 28.02.2017


·         WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA WAKIWA NA SAMAKI WACHANGA KIASI CHA   500 KG, WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA MNAMO TAREHE 28.02.2017 MAJIRA YA SAA 04:00HRS ALFAJIRI KATIKA MWALO WA ZIWA VICTORIA MAENEO YA KAMANGA FERI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATATU WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1. SHINJE LOMELO, MIAKA 34, MSUKUMA NA MKAZI WA IGOMA, 2. DANIEL SIMON MIAKA 40, MKAZI WA IGOMA NA 3. SEMU JIMMY MIAKA 50, MNYAKYUSA NA MKAZI WA ILEMELA, WOTE WAFANYABIASHARA WA SAMAKI,  KWA KOSA LA KUPATIKANA NA SAMAKI WACHANGA KIASI CHA  KILO GRAMU 500, KITENDO AMBACHO NI KINYUME KISHERIA.

AWALI ASKARI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA USIKU KATIKA MWALO WA ZIWA VICTORIA WAPO BAADHI YA WATU WAVUVI WANAOFANYA BIASHARA  HARAMU YA KUUZA SAMAKI WACHANGA KWA WAFANYA BIASHARA, AIDHA  BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIZO ASKARI WALIANZA KUFANYA UFUATILIAJI KWA KUFANYA DORIA NA MISAKO  KATIKA MAENEO YOTE YA MWALO WA ZIWA VICTORIA.

AIDHA ASKARI WALIENDELEA UFUATILIAJI NDIPO LEO TAREHE 28.02.2017 MAJIRA TAJWA HAPO JUU ASKARI WALIWAKAMATA WATUHUMIWA WATATU TAJWA HAPO JUU WAKIWA NA SAMAKI WACHANGA KIASI CHA KILO GRAMU 500 WALIOVULIWA NA ZANA  HARAMU ZA UVUVI KOKORO, AMBAO HAWARUSIWI KUVULIWA KISHERIA .

WATUHUMIWA WOTE WATATU WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMNI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO, AIDHA POLISI WANAENDELEA NA MISAKO PAMOJA NA DORIA KATIKA MAENEO YOTE YA MWALO WA ZIWA VICTORIA ILI KUWEZA KUDHIBITI UHALIFU KATIKA MAENEO HAYO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MASNGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WAVUVI AU WAFANYABIASHARA AMBAO WANAENDELEA KUFANYA UVUVI HARAMU, ILI WAWEZE KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.