NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
WAKATI sakata la dawa za kulevya likipamba moto nchini Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na misokoto 59 ya bangi pamoja na madawa yanayodhaniwa kuwa ni ya kulevya yaitwayo kabasanda kiasi cha kilo moja.
Tukio hilo limetokea February 14 mwaka huu saa 11 jioni maeneo ya Nyakato kata ya Nyakato Wilaya ya Nyamagana Mkoani hapa ambapo askari wakiwa kwenye doria na misako walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa watu hao.
Akiwataja watuhumiwa hao mbele ya waandishi wa habari jana Naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi alisema kuwa ni Vitarius Mtasingwa (35) , Bhoke Sam (36), Alladini Hussein (44) wote wakazi wa Nyakato National
Ameeleza kuwa awali askari wakiwa kwenye misako na doria walipokea taarifa kutoka kwa raia kuwa kuna watu wanaosadikika kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na kwamba askari walifanya ufuatiliaji wa haraka maeneo hayo na kufanikiwa kuwakamata wote watatu.
Aidha amesema kuwa baada ya tukio hilo askari waliendelea na doria katika maeneo tofauti ambapo ilipofika saa 01.30usiku February 15,mwaka huu maeneo ya hotel Mwanza Wilaya ya Nyamagana , askari walifanikiwa kumkamata mtummoja aliyejulikana kwa jina la Mwalimu Mohamed (30), mkazi wa Kirumba akiwa na noti 46 za sh Elfu kumi zenye jumla ya thamani ya sh 460,000kitendo ambacho ni kosa la jinai.
“Wakati huo askari wetu wakiwa doria katika maeneo hayo walipata taarifa ya kutoka kwa raia wema kwamba yupo mtu ambaye walimtilia shaka kwamba ni mhalifu ndipo askari wafika kwenye eneo hilo na kuweza kumkamata”alisema Msangi.
Aidha polisi wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote wanne, na kwamba taratibu zinafanya zinafanyika za kupeleka mimea ya kabasanda iliyokamatwa kwa mkemia wa serikali ili kuweza kubaini kama ni madawa ya kulevya au laa , pindi uchunguzi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani na kwamba misako ya kuwatafuta watu wengine ambao wanadaiwa kushirikiana na watuhumiwa tajwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.