ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 15, 2017

MWANAMUZIKI WA MUZIKI ASILI ANASWA NA MENO YA TEMBO


Kukutwa na nyara za serikali.
Na James Timber, Serengeti
Mwanamziki wa wimbo wa Magina Ndare  maarufu kwa jina la Surambili na wenzake wanne wamefikishwa katika mahakama ya wila ya Serengeti, kujibu tuhuma za kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya sh,milioni 33,000,000.


Mwendesha mashitaka wa Jamhuri Emanuel Zumba,mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Ismael Ngaire amewataja  watuhumiwa  kuwa ni Paulo Ryoba Mwita (38) mkazi wa Gesarya, Joseph Ghati Masero (49) mkazi wa Machochwe, Mwita Mwita Masero (51)mkazi waMachochwe, George Samwel Sura mbili mwenye miaka(44)mkazi wa Mikomarilo na PetroMwikwabe (42) mkazi wa Merenga.


Akisoma mashitaka, Zumba amesema kuwa kosa la kwanza ni kuingia ndani  ya korongo la Nyegena ililoko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,januari13 majira ya usiku ambapo ni kinyume  cha kifungu cha21 (1) (2)a cha sheria za uhifadhi Tanzania sura ya 282 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


Kosa la pili ni  kufanya shughuli ya uwindaji ambapo ni kinyume cha kifungu cha23 (1) (2)a cha sheria za uhifadhi Tanzania sura ya 282 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


na kosa la tatu ni kujihusisha kuwa na nyara  za serikali ambapo januari18mwaka huu katika kijiji cha Machochwe watuhumiwa walikutwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya sh,milion33,000,000 wakisafirisha kwenda Isbania ambapo ni kinyume cha kifungu cha 84(1)(2)acha sheria namba5 ya mwaka 2009.


Hata hivyo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote,na wako mahabusu hadi Februari 23 kesi hiyo itakapo tajwa tena.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.