Mwana wa nguli wa masumbwi duniani marehemu
Muhammad Ali, alikumbwa na adhaa baada ya kutiwa mbaroni katika uwanja
wa ndege wa jimbo la Florida kwa kuwa na jina la Kiislamu.
Muhammad Ali Junior, mmoja wa watoto wa marehemu Muhammad Ali,
alitiwa mbaroni katika uwanja wa ndege wa jimbo la Florida wakati
alipokuwa akirejea kutoka nchini Jamaica kuingia Marekani. Habari zaidi
zinasema kuwa, baada ya kutiwa mbaroni mwana huyo wa Muhammad Ali
alihojiwa kwa masaa mawili.
|
Marehemu Muhammad Ali enzi za uhai wake akiwa na mke wake Khalilah Camacho Ali. |
Muhammad Ali Junior alizaliwa katika mji wa Philadelphia katika jimbo
la Pennsylvania nchini Marekani huku akiwa na pasi ya kusafiria ya nchi
hiyo. Junior anaishi nchini Jamaica pamoja na mama yake, Khalilah
Camacho Ali. Wakili wa mwana huyo wa Muhammad Ali, kwa jina la Chris
Manshny amesema kuwa kijana huyo wa mwanamasumbwi mashuhuri duniani na
mama yake walitiwa mbaroni katika uwanja huo wa ndege wa Florida mwezi
huu kutokana na kuwa na majina ya Kiarabu.
|
Uwanja wa ndege wa Florida wakati mwana huyo wa Muhammad Ali alipotiwa mbaroni. |
Kwa mujibu wa wakili huyo, Bi, Khalilah Camacho Ali na mwanaye
waliachiliwa, mara baada ya kuonyesha picha inayomuonyesha yeye akiwa na
marehemu mume wake huku wakiwa tayari wamehojiwa kwa muda usiopungua
masaa mawili. Tangu Rais Donald Trump wa Marekani aliposaini marufuku ya
kuzuiwa raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini humo, Waislamu
wamekuwa wakikumbwa na madhila mbalimbali ndani ya taifa hilo
linalojinadi kuwa mtetezi wa haki za binaadamu duniani. Hii ni katika
hali ambayo mahakama kadhaa za nchi hiyo zimetaka kutupiliwa mbali
marufuku hiyo ya Rais Trump.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.