Na James Timber, Mwanza
Msanii chipukizi wa Kizazi kipya Bongo flava Kabanza kutoka jijini Mwanza, ametambulisha leo kibao chake kipya kiitwacho Digital alichomshirikisha Ydee kilichotengenezwa na Adolf Beatz pamoja na producer Doucher Master.
Kabanza itakuwa Track yake ya tatu baada ya kibao chake cha kwanza kilichomtambulisha kiitwacho Money na cha pili Mdananda alichokifanya mwaka jana akishirikiana na Ydee ambacho kilikuwa hit kwenye media za jijini hapa kutokana na Ujumbe, uliokuwemo, Melody na Beatz
Msanii huyo mwenye jina lake halisi Kabanza Peter ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma anayechukua Degree ya Chemistry, alipenda mziki toka anasoma shule ya msingi na kujiingiza kwenye vikundi vya sanaa shuleni alipokuwa O’level pia na kufanya vizuri Shule ya Sekondari Bugogwa iliopo Ilemela jijini Mwanza.
Aidha aliomba watanzania wapenda mziki wa kizazi kipya bongo flava kumpa sapoti kadri wawezavyo ili kumfikisha sehemu anayostahili.
“Nimeachia Kibao changu kipya leo February 1, 2017 kiitwacho Digital nilichomshirikisha Ydee, naomba washabiki na wapenda mziki wa kizazi kipya wakipokee wasikilize na pia naomba wadau wanisapoti ili nifike mbele zaidi,” alisema Kabanza.
Kwa upande wake Msanii huyo anaamini heshima na nidhamu ndio nguzo bora katika kufanya vizuri na kupaa juu zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.