Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es Salaam imeridhia ombi la upande wa jamhuri lililokuwa likiiomba mahakama kuwaweka chini ya uangalizi watuhumiwa 13 wa dawa za kulevya waliofikishwa mahakamani hapo na kusoimewa hati ya ombi hilo kwa mahakimu wawili tofauti katika mahakama hiyo.
T.I.D, Recho, Petitman na wengine ni baadhi ya waliokuwa wameshikiliwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kwa mahojiano kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.
Taarifa ni kwamba wameachiwa kwa dhamana ambapo moja ya masharti waliyopewa ni kuripoti Polisi mara mbili kwa mwezi ambapo TID, Recho, Tunda, Nyandu Tozy, Babuu wa kitaa na Rommy Jones watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana yao ni milion 10 kila mmoja.
Petitman na wenzake watatu wao watakuwa kwa uangalizi wa polisi kwa miaka mitatu na dhamana ya kiasi cha milioni 20 kila mmoja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.