Makumi ya wahajiri wanahofiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kwenda bara Ulaya kuzama katika Bahari ya Mediterranea.
Gadi ya Pwani ya Italia imesema kuwa, boti hiyo iliyozama ilikuwa imebeba wahajiri 110 waliokuwa wakielekea barani Ulaya kuomba hifadhi. Taarifa ya gadi hiyo imeongeza kuwa, boti hiyo imezama yapata kilomita 50 pwani ya Libya na kwamba timu za waokoaji na wapiga mbizi zinaendeleza juhudi za kutafuta manusura na miili ya wahajiri hao.
Habari zinasema kuwa, miili 13 pekee ndiyo imepatikana kufikia sasa lakini juhudi za kutafuta wahanga wa ajali hiyo zinaendelea kufanywa na jeshi la majini na angani la Italia, Uhispania na Ufaransa.
Boti iliyobeba wahajiri zaidi ya 240 ikizama katika Bahari ya Mediterranea mwaka jana |
Hivi karibuni, Shirika la Kimataifa la Uhajiri (IOM) lilisema wakimbizi na wahajiri zaidi ya 5,000 walipoteza maisha mwaka jana wa 2016 wakijaribu kuingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterranea.
Naye William Spindler, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema kiwango hicho cha vifo baharini mwaka jana kimevunja rekodi na kwamba hakuna mwaka ambao umewahi kushuhudia vifo vya wahajiri baharini kiasi hiki.
Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Italia, wahajiri wapatao 181,000 waliokuwa wakitokea Libya waliingia nchini humo mwaka uliopita kuomba hifadhi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.