Madola mawili ya Ulaya, Ujerumani na Uswisi nayo yamejiunga na safu ya wapinzani wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Serikali ya Ujerumani imetoa taarifa yenye lugha kali na kukemea hatua ya Israel ya kupasisha mpango wa kujenga nyumba mpya 2500 za walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za palestina.
Martin Schaefer, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Ujerumani sambamba na kukemea hatua hiyo amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo ina wasiwasi kama kweli Israel inafuatilia malengo rasmi na makubaliano ya huko nyuma na Wapalestina.Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel anayeongoza kwa kasi mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina. |
Aidha Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uswisi nayo imetoa taarifa inayokemea na kulaani vikali uamuzi wa Israel wa kutaka kujenga nyumba mpya 2,500 katika Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds inayokaliwa kwa mabavu.
Taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uswisi imeeleza kuwa, kuendelea siasa za ujenzi wa vitongojo vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina ukiwemo mji wa Quds ni kikwazo katika njia ya kufikiwa amani huko Palestina.
Ikumbukwe kuwa, licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomeshe ujenzi wa vitongoji katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, utawala huo ghasibu umeidhinisha ujenzi wa nyumba nyingine mpya 2,500 katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.