Mmoja kati ya wadau wa soka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu David Burhan ambapo wapenzi wa soka jijini Mwanza wamehudhuria ibada fupi ya kuuaga mwili wa marehemu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, na kisha kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Iringa. |
WAKATI HUO HUO TFF YATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI.
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mchezaji wa Kagera Sugar, David Abdalla Burhan kilichotokea Hospitali ya Bugando usiku wa kumkia Januari 30, 2017.
Kutokana na kifo hicho, Rais wa TFF ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi mzima wa Klabu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, familia ya marehemu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa marehemu Burhan.
Taarifa za awali, zilisema kwamba kabla ya umauti, Burhan aliugua ghafla wiki iliyopita akiwa safarini kutoka Singida na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo usiku wa Alhamisi.
Siku ya Ijumaa alihamishiwa Hospitali ya Kagera Sugar, na kisha kusafirishwa hadi Bugando siku ya Jumapili kwa uchunguzi zaidi. Usiku wa Jumapili, alifanyiwa vipimo na kuonekana kwamba mapafu yamejaa maji. Katika jitihada za kupatiwa matibabu alifariki saa nane za usiku wa Jumapili.
Mwili wa marehemu umeagwa leo na wapenzi wa soka jijini Mwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, na kisha kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Iringa.
Kwa mujibu wa familia mazishi yatafanyika kesho Jumatano Februari mosi.
Marehemu enzi za uhai wake. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.