MBUNGE wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula, amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya cha Sangabuye kilichopo kata ya Sangabuye Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, alikabidhi gari hilo jana kwenye kituo hicho kwa ufadhili wa Shirika la Afya Duniani kupitia Wizara ya Afya nchini kwa ajili ya kuimarisha huduma za Afya.
Akieleza sababu za kupeleka gari hilo kituoni hapo mbele ya wananchi amesema kutokana na idadi ya watu wanaopata huduma za Afya pamoja na maeneo visawani wanaopatibiwa kwenye kituo hicho tofauti na vituo vingine vilivyopo kwenye manispaa hiyo.
“Najua mtajiuliza kwanini gari limeletwa kituo cha Sangabuye na sio kingine, nimefanya hivyo kwa sababu nafahamu kituo hiki kinahudumia watu wengi na kinatoa huduma ya upasuaji, hivyo kina uhitaji mkubwa wa gari la wagonjwa lenye huduma zote lakini pia litafanya kazi hata katika vituo vingine na sio Sangabuye peke yake”amesema Mabula.
Ameeleza kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na zenye uhakika huku akiwasihi watu watakao tumia gari hilo kuhakikisha linafanya kazi iliyokusudiwa na sio kitu kingine kama ambavyo baadhi ya maeneo wamekua wakilitumia kama kubebea miziko ya samaki.
Awali akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya kituoni hapo Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dkt. Wilfred Rwechungura kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Wanga, ameeleza katika kuboresha upatikanaji wa huduma kwa jamii, mpaka sasa Halmashauri ina jumla ya vituo 44 vya kutolea huduma za Afya, zahanati 31, vituo vya Afya 12 na hospitali moja huku kituo cha Sangabuye kikiwa moja kati ya vituo vya Afya kinachotoa huduma kwa kata tatu za Sangabuye, Kayenze, Bugogwa na wilaya ya Magu.
“ Pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wetu lakibi bado halimashauri ina changamoto ya uhaba wa watumishi kwani mpaka sasa kuna jumla ya watumishi wa Afya kada mbalimbali wapatao 319 huku uhitaji ukiwa ni 606 hivyo kufanya upungufu wa watumishi 287 sawa na asilimia 47.4” amesema Rwechungura.
Hata hivyo Mbunge Mabula amesema suala la Ajira liko mbioni kukamilika na hivyo kuanza kutolewa muda si mrefu hususani Afya na Elimu na kwamba hizo ndizo zitakazopewa kipaumbela.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.