Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika Feb 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Meshack Mwankemwa wa Mbeya |
Na Mwandishi Wetu
Bondia Meshack Mwankemwa wa Mbeya ameingia jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri mpambano utakaokuwa wa raundi kumi za ubingwa wa EAST/ CENTRAL AFRICA siku ya Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi
akizungumza na wahandishi wa habari Promota wa mpambano uho Sadick Kinyogoli amesema kuwa huu ni wakati wa mwisho wa kuelekea mpambano wenyewe mana utafanyika mwishoni mwa wiki hii
aliongeza kwa kusema Mwankemwa ametuwa jijini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na Shauri ndio kwao hivyo mpambano utakuwa mkali sana kwa kuwa mabondia wote wameshacheza mapambano makubwa ya kimataifa hivyo wapenzi waje mapema kuangalia burudani ya mchezo wa masumbwi walioikosa kwa kipindi cha nyuma
katika mpambano huo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kusindikiza mtanange uho
Kinyogoli alisema kuwa bondia Mohamed Matu,mla atapambana na Mfaume Mfaume wakati bondia chipkizi anaekuja kwa kasi katika mchezo uhu wa masumbwi Iddi Mkwela ataoneshana umwamba na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi zisizokuwa na ubingwa
mchezo mwingine wa ubingwa wa taifa utakuwa kati ya Said Chino na Twalib Tuwa ubingwa wa taifa wa TPBC mkanda ambao unatetewa na Tuwa Husein Pendeza wa Ashanti Boxing clab ya Ilala atakaevaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Conetion na Mbwana Matumla atazichapa na Suleimani Shabani
pamoja na mpambano mwingine wa kimataifa wa kina dada Anisha Bashir kutoka Malawi na Ester Boazi Kazeba wa Tanzania
aliongeza kwa kusema kuwa mabondia wote watapima uzito pamoja na Afya zao siku ya feb 4 katika hotel ya Atrium iliyopo sinza Afrika sana hiyo mabondia wote watakuwa pale jumamosi kwa ajili ya upimaji uzito pamoja na Afya zao
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.