MABINGWA watetezi wa taji la VPL wamerudi kileleni mwa ligi mara baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mwadui FC na kufikisha pointi 46 pointi moja mbele ya watani wao wa jadi Simba SC.
Obrey Chirwa ndio shujaa wa mchezo huo baada ya kufanikiwa kufanikiwa kufunga magoli yote mawili dakika ya 71 na 85 kipindi cha pili yaliyoipa Yanga ushindi na kuifanya iongoze msimamo wa ligi.
Chirwa aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima na kufanikiwa kufanya kweli kuipa timu yake ushindi muhimu iliokuwa ikiuhitaji ili kuitoa Simba kwenye nafasi ya kwanza baada ya kupoteza mchezo wake wa jana dhidi ya Azam.
Mwadui FC walijitahidi kupambana kuizuia Yanga wakiongozwa na wachezaji wazoefu kama Nassoro Masoud ‘Cholo’, Awadh Juma, Shabani Kado na wengine.
Yanga walikuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wao dhidi ya Mwadui na walihitaji ushindi pekee ili ili kuiondoa Simba kileleni mwa ligi.
KIKOSI CHA YANGA.
Deogratias Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Justine Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amis Tambwe, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke.
BENCHI
Beno David, Oscar Joshua, Said Juma, Yussuf Mhilu, Obrey Chirwa, Emanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya.
KIKOSI CHA MWADUI FC
Shabani Kado, Iddy Mobby, Nassoro Cholo, Yassin Mustapha, Malika Ndeule, Hassan Kabunda, Razack Khalphani, Awadh Juma, Paul Nonga, Salim Khamis na Abdala Seseme.
BENCHI
Lucheke Mussa, Salum Kanoni, David Luhende, Shabani Aboma, Meshack Meshack, Jerryson Tegete na Joseph Kimwaga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.