ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 27, 2017

APIGWA MAWE HADI KUFA KISA KUIBA KUKU.

Apigwa mawe hadi kufa kisa kuiba kuku.
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Safari Bungate mwenye umri wa miaka 51, mkazi wa kijiji cha Kanyelele wilayani Misungwi Mkoani Mwanza ameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili na kundi la watu walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa madai ya kuiba kuku.

Tukio hili limetokea jana TAREHE 26.01.2017 majira ya saa 04:00 usiku,baada ya kuiba kuku nyumbani kwa Tetema Mathias (40) ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji hicho. 

Taarifa zaidi zinasema kuwa mnamo majira hayo tajwa hapo juu, mwenye nyumba Bwana Tetema akiwa amelele na familia yake, marehemu alifika kwenye nyumba hiyo na kupitia dirishani alizama ndani na kisha kuiba kuku mmoja.

Bwana Mathas alisikia vishindo vya kimya kimya vya kunyemelea visivyo vya kawaida na mara baada ya kunyanyuka toka kitandani kuelekea mahala sauti za chini zilikuwa zikisikika  akamnasa mwizi wake n kuanza kupiga yowe akiomba msaada wa majirani.

Marehemu Safari aliponyoka mikononi mwa bwana huyo akikimbia barabarani ambako alikamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuanza kushambuliwa na mawe akichapwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili hadi kupoteza fahamu na baada ya muda akazimika.

Raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi, nao askari wakafika eneo la tukio na kukuta mtuhumiwa wa wizi huo akiwa tayari amefariki. 

Mwilia wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwaajili ya mazishi.

Aidha bwana Tetema Mathias aliyeibiwa kuku anashiiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, AIDHA ANAWATAKA WANANCHI PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU WAMFIKISHE KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE. 
HABARI NA GSENGO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.