Daladala zinazo fanya safari kati ya Tegeta Nyuki zikiwa zimesongamana katika Kituo cha Daladala nje ya geti Kuu la Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam juzi baada ya kupangiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchikavu na Majini (SUMATRA) yawe yanashusha na kupakia hapo na kusababisha adha kubwa ya abiria na madereva hao walitii nakuyapeleka magari yao Muhimbili kama walivyo elekezwa na (SUMATRA) nakumfanya Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi, Adnan Kondo kuwaamuru waondoke na warudi walikotoka
Hapa abiria wakishuka katika mabasi hayo ya Daladala juzi.
(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga (kulia) akizungumza jambo Dar es Salaam jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya mabasi vya Muhimbili, Feri na Gegerezani akiwa amwongozana na Viongazi mbalimbali wa SUMATRA, Wamiliki wa Mabasi hayo, Madereva na Wenyeviti na makatibu hasa wanjia ya Tageta kujionea hali halisi na changamoto ili waweze kuzitolea majawabu
Ofisa leseni na Udhibiti Usafiri wa barabara Mkoa wa Dar es Salaam, Bernard akilipiga picha Gari Moja lilofika kwa majaribio katika Kituo cha Mabasi cha Muhimbili
Kaimu Katibu wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala (katikati aliyevaa miwani) akizungumza jambo wakati wa Ziara ya Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga kutembelea maeneo mbalimbali ya vituo iliwemo Kituo cha Daladala cha Muhimbili ambapo alianzia hapo na kutembelea Feri na Gerezani Dar es Salaam jana
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga (kulia) akizungumza jambo wakati walipofika katika Kituo cha Mabasi cha Feri kwa lengo la kujionea changamoto mbalimbali
Kituo cha Gerezani Daladala Zikiwa zimesongamana huku wakiwa wanapakia Abiria kwa zamu
Mwenyekiti wa Daladala Zinazofanya Safari ya Tegeta Nyuki (Gosbart mushaka) akizungumza jambo wakati Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani Ilala, Peter Mashishanga kufika katika Kituo cha Gerezani na Timu yake kujionea hali halisi zilizopo kituoni hapo na aweze kujadiliana na viongozi mbalimbali na kulipatia jawabu swala la Daladala za Tegeta Nyuki ambazo awali zilikuwa zikipaki Kariakoo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.