Mmoja wa wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza akifurahia kurejea katikati ya jiji kufanya biashara baada ya tamko la Mhe. Rais JPM. |
Akinamama wauza mbogamboga na vijana wa matunda na wale wauzanguo nao wameungana shereheni. |
Shangwe ingawa mfukoni ni dhaifu............... |
Maisha mapya mitaa iliyokuwa imejaa mishemishe ya Makoroboi jijini Mwanza. |
Mahesabu na tafakari. |
Shangwe za vijana wake kwa waume mitaa ya Makoroboi. |
HABARI: ANNASTAZIA MAGINGA,
PICHA: ZEPHANIA MANDIA
GSENGO BLOG. Mwanza
WAFANYABIASHARA ndogondogo (Machinga)Jiji la Mwanza wamepokea kwa furaha tamko la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzanaia Dk. John Magufuli baada ya kuwaruhusu kurudi katikati ya jiji kuendelea na biashara zao bila kubugudhiwa.
Tamko hilo limetoka baada ya siku tatu halmashauri ya jiji la Mwanza na manispaa ya Ilemela kuwaondoa machinga mjini na kuwapeleka kwenye maeneno yaliyoruhusiwa hali iliyowathiri wafanyabiashara hao.
Machinga hao wakizungumza na GSENGO BLOG kwa wakati tofauti wamesema kurudi mjini kuwawasaidia kuongeza uchumi kutokana na mzunguko wa watu .
Mmoja wa machinga hao Abdul Mwinyi amesema Rais amefuata haki kwa sababu aliahidi ajira kwa vijana na kuwasaidia machinga na kwamba kwa tamko hilo limewatoa njia panda.
“Jamani ilikuwa imetuathiri sana mana wengine tumekuwa tumezoeleka na watu lakini siku hizi tatu tumehaha hali ikawa ngumu ya uchumi lakini mimi binfsi namshukuru Rais.”amesema Mwinyi
Naye Closper Gozibert amesema anashukuru Rais kwa kuliona hilo lakini huku pia akijifunza kuwa kwenye watendaji wake alionao wengi wao wanafanya kazi kwa mihemko bila kujali athari za wananchi .
Aidha Mapema kabla ya tamko la Rais Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ya Nyamagana na manispaa ya Ilemela kuboresha miundo mbinu kwenye maeneo ya waliohamishia machinga ili kuhakikisha yanakuwa ya kudumu.
Mongella pia amesema maeneo yapo ya kutosha kwani Buswelu yapo maeneo 400 na kuwapangia machinga kukaa kwenye maeneo yao huku serikali ikiwa na mpango wa kuwawezesha mikopo vijana na wakina mama.
Aidha Mongella ameongeza kuwa melekezo ya Rais ilikuwa ni kuwaondoa wamachinga na kuwapeleka kwenye maeneo yao ndiyo yalikuwa yanawasumbua na kwa sasa wameweza kuyatekeleza.
MASWALI YA GSENGO BLOG NA GSENGO
Yote 9, Kumi nini Hatma ya waliovunjiwa vibanda vyao na vitendea kazi vyao vilivyoharibika na kuteketea wakati wakinusuru mali zao.
- Haki iko wapi juu ya unyanyasaji wa hali ya juu uliojitokeza ndani ya zoezi? Pamoja na baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kusema zoezi liliendeshwa kwa amani na utulivu lakini baadhi ya manung'uniko na vitendo vya vya unyanyasaji vya waziwazi vilivyokuwa vikifanyika, manyanyaso, udhalilishaji ikiwamo watu kupigwa na kuumizwa hata wengine kukamatwa na kutupwa ndani?
- Mgambo waliotumika walikuwa hawana simile wameleta maumivu makubwa kwa raia kiasi gani?
- Nimepita pale eneo la Ghana wilayani Ilemela na kufanyapia tathimini za kuzihoji baadhi ya kaya viunga vya mitaa ya Uhuru na vilima ya Igogo wilayani Nyamagana kuna mitaa ambapo kati ya kila nyumba 10 nyumba 8 zina akinamama wajane na nyumba 2 zinazobakia ni akinamama wenye waume zao walio hai.
Hawa akinamama 8 wote wanaendesha maisha yao na watoto walioachwa na marehemu waume zao kwa biashara za maandazi, vitumbua, matunda, nguo za mitumba na biashara nyingine za mitaji ya chini ya shilingi elfu 50 na hizi ndizo zinazo walisha wao na watoto wao.
- Vipi kwa vijana mafundi garage, waziba pancha na wapaka rangi magari waliokuwa wamejiajiri mitaani, nao wakahamishiwa eneo la Sabasaba umbali wa kilomita 10 toka katikati ya mji ambako nako hapakutosha?
- Hapa sijagusia kuhusu vijana walioishia darasa la saba na hata wale waliomaliza kidato cha nne na wale wa vyuo wasio na ajira = BOMU JIPYA LILIKUWA LINAPIKWA HAPA.
Jeh wameathirika kwa kiasi gani kwa hizi siku 3 za kuwaondoa barabarani?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.