ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 29, 2016

NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA 3 VIJIJI VYOTE WILAYA YA UKERERE KUWA NA UMEME.

NA ALBERT G SENGO
UKEREWE.

Waziri wa Nishati na madini Profesaa Sospita Muhongo amesema tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza litamalizika ndani ya muda wa miaka mitatu baada ya kuvipatia huduma ya umeme vijiji 38 ambavyo bado havijapata nishati hiyo.

Profesa Muhongo ametoa kauli wakati akizungumza na wakazi wa vijiji mbalimbali katika wilaya ya Ukerewe na kuwaomba kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuwapelekea huduma ya Umeme.

Mradi wa REA 2 umekamilika katika vijiji 38 kati ya 76 vya wilaya hiyo.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo amekagua utekelezaji wa mradi huo na kukutana na kilio cha wananchi ambao hawajaunganishiwa umeme licha ya nishati hiyo kufika kwenye vijiji vyao.

"Kaya kama nne tu ndizo zilizobahatika kupata umeme lakini kijiji cha mkoko kinatakribani kaya kuanzia elfu mbili na hivyo tunaomba umeme na sisi utufikie" Alisema mmoja wa wananchi.

 Profesa Muhongo akatumia mwanaya huo kuwaondoa hofu wananchi "Lakini Ukere tulishasema ndani ya kipindi cha miaka mitatu tutakuwa tumelitatua tatizo walilonalo, Meneja wa Kanda hebu tuambie mliyoyazungumza na mmefikia wapi....." BOFYA PLAY KUSIKILIZA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.