Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) akihutubia mamia ya wananchi jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kata ya Igoma Wilaya ya Nyamagana lengo likiwa ni kumshukuru Rais Dk John Magufuli kuwarejesha wamachinga kufanya shughuli zao maeneo ya Mjini. |
MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) amedai yuko tayari kuchangia gharama ya mawakili watakaowekwa na wafanyabiashara wadogo maarufu machinga ili kuwafungua kesi ya kudai fidia Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Mabua alitoa kauli hiyo jana jioni wakati akihutubia mamia ya wananchi waliofulika katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Igoma Sokoni kwa lengo la kumshukuru Rais Dk John Magufuli kwa hatua yake ya kuwarejesha machinga kuendelea na shughuli zao maeneo ya mitaa ya Mjini katika Jiji la Mwanza ikiwa ni baada ya kuondolewa kwa nguvu.
“Rais Dk Magufuli amekuwa Musa wetu kama yule aliyewaokoa wana wa Taifa la Israel, kwani machinga ni watu wanyonge wanaohangaika kujitafutia lidhiki katika mazingira magumu lakini Mkurugenzi wa Jiji, Kiomoni Kibamba na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha wakapuuza ushauri wa Baraza la Madiwani wa Jiji na viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa wakawaondoa kwa nguvu tena bila huruma,”alisema.
Mbunge huyo akizungumza kwa hisia kali katika mkutano huo alisema kwamba kitendo kilichofanywa na Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kilirenga kuwaongezea umasikini kutokana na kufanya zoezi la kuwaondoa wakati wa usiku na hata walipowatoa mjini kati waliendelea kuwafuata hata maeneo ya nje ya mji kama Igoma, Mkuyuni, Mkolani na Buhongwa.
“Waliwaondoa mjini kati lakini wakadai wamewatengea maeneo ya kufanyia shughuli zenu cha ajabu nako wakawavunjia bira huruma huu ulikuwa ni unyama, Mimi kama Mbunge kazi yangu ni kushughulika na matatizo ya watu hivyo hivyo Chama cha Siasa na Serikali kisiposhughulika na kero za wananchi haikitaungwa mkono na serikali ikiwa madarakani itakataliwa wakati wa uchaguzi,”alisema.
Mabula alimtaka Mkurugenzi Kibamba kushirikiana na madiwani wa Jiji hilo ambao waliidhinisha kiasi cha Sh milioni 60 kwa ajili ya kuboresha eneo la Community Center lililopo Kata ya Mirongo, Sinai lililopo Kata ya Mabatini na Nyegezi ili kuwekewa miundombinu ya vyoo na mabanda ya mamalishe ili kuweza kuhamishiwa baadhi ya wamachinga na sio kuwatoa .
“Tangu Rais Dk Magufuli amteuwe Kibamba kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na kuwasili kutekeleza majukumu yake amekuwa mtu wa migogoro tu mkumbuke alianzisha mgogoro na Walimu wakuu wote wa Shule za msingi na sekondari, alitangaza kuwanyang’anya wenyeviti wa mitaa 175 mihuri, alitaka kuvunja nyumba 217 mtaa wa Ibanda na aliondoa wamachinga mjini,”
“Hataki ushauri wa baraza la madiwani hamsikilizi Meya wa Jiji, James Bwire, Naibu Meya, Bikhu Kotecha, Madiwani anasema hao ni wanasiasa haelewani na Mbunge Mabula hata viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya ataki kuwasikiliza amekuwa akitamba kuwa yeye ni Mwanasheria makini sasa huyu atafanya kazi na nani ?,” alihoji Mabula huku wananchi wakipaza sauti wakitaka aondolewe.
Mbunge huyo pia alisikiliza kero mbalimbali za wananchi ambapo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Igoma Kati, Jackison Kato alimweleza Mabula kuwepo kiongozi wa soko la Igoma alikuwa akiwatoza wananchi zaidi ya 200 waliokibilia hapo baada ya kuvunjwa vibanda vyao wakati wa zoezi la kuondoa machinga ambapo aliwatoza Sh 10,000/- kila mmoja hivyo kujipatia kiasi zaisi ya Sh milioni 2.
Mabula aliamuru kiongozi huyo wa soko aliyetajwa kwa jina la Mawazo Mazigo kurejesha mara moja fedha hizo kwa wananchi na asipofanya hivyo atachukuliwa hatua na ikiwemo kuahidi kupita Kituo cha Polisi baada ya kumaliza mkutano ili kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Nyakato waweze kumkamata ili awarejeshee fedha wananchi alizovchukua kinyume na utaratibu wa Halmashauri ya Jiji.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nyamagana kata ya Igoma. |
Mbele ya Kusanyiko Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stansalaus Mabula pia alitoa nafasi ya wananchi kuuliza maswali.. |
TASWIRA YA MWANZA KUFIKIA 2020
Ni wazi kuwa si barabara kuu tu zitakuwa kiwango cha lami na ujenzi wa mawe bali pia barabara za ndani kwenye mitaa ya makazi ya watu nazo ziko kwenye mpango.
Barabara korofi ya Isamilo, Kawekamo iliyopita Nyakabungo, Barabara za Pamba, Bugando, Bugarika zote lami. Jeh nikupitia fedha zipi mpango wa ujenzi utaanza lini BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Kuanyiko la wananchi Igoma. |
Ward ya wanaume ni tatizo, fedha tayari zimeshatengwa, mwakani kuna mjengo wa ghorofa mbili utaporomoshwa katika hospitali ya wilaya.
Nyamagana kwa kipindi kirefu imekuwa na uhaba wa gari la kusafirisha wagonjwa hivyo ambulance yaja BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Hasara kubwa imejitokeza uchinjaji ng'ombe umeshuka toka ng'ombe 300 kwa siku hadi ng'ombe 50. Na hapa Mhe. Mabula anatuma salamu kwa waziri wa Mifugo.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
SASA NI WAKATI WA MASWALI NA MAJIBU.
Mwananchi Mathew Manyonyi. |
Boniface Nkobe Mkazi wa Igoma aliuliza swali juu ya gharama zilizotumiwa na Halmashauri kwa operesheni ya ondoa machinga Jeh ni shilingi ngapi zimetumika kwa oparesheni hiyo? |
Mzee huyu anadai fidia kwa kiwanja chake kilichobadilishwa matumizi na Halmashauri. |
Chausiku Mstapha mama huyu ni muhanga ambaye nyumba yake iliyoko Kishiri A ilivunjwa kupisha upanuzi wa soko ambapo huko wa machinga walihamishiwa nini hatma yake. SWAI LAKE NA JIBU LIKO CHINI KWENYE PICHA YA MBUNGE. |
Taa za barabarani ziliwekwa kwaajili ya nini...na ni kwanini hazijawaka yapata mwaka sasa? MAJIBU YA MBUNGE YAKO CHINI YA PICHA YA MBUNGE INAYOFUATA. |
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula juu ya jukwaa akijibu maswali aliyoulizwa na wananchi kutoa ufafanuzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kata ya Igoma Wilaya ya Nyamagana. |
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akisaini kitabu cha mahudhurio kata ya Igoma baada ya kumaliza mkutano katani humo. |
Miaka ya sasa wananchi wako makini sana, na hapa walikuwa wakirekodi matukio mbalimbali yakiwemo majibu ya maswali waliyouliza na yakapata ufafanuzi. |
Mabula ametoa ushauri kwa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza ikiwemo ile ya Jimbo lake Halmashauri ya jiji la Mwanza, Kwamba Shughuli ya kuhama ifanyike kwa awamu na hatua:-
Wananchi wenzangu wa Nyamagana tunajua ya kwamba serikali kuu chini ya Rais magufuli inahamia Dododma. Utagundua ya kwamba hekima za raisi ni kufanya mambo kwa utaratibu, pamoja na kwamba shughuli hii ni nyeti na yenye tija kwa Taifa lakini inafanyika kwa awamu na hatua.
Ninaikumbusha Halmashauri ya jiji la Mwanza na wataalamu wote ya kwamba hakuna jambo kubwa, nyeti na muhimu kama hili ambalo hufanyika ndani ya usiku mmoja (overnight) - Hakuna!
Hivyo basi wataalamu wakae na kuweka awamu na hatua za kuhama kwa kuimarisha miundo mbinu, kuandaa mazingira na kuwaandaa wafanyabiashara na wanannchi wote kisaikolojia ili kujenga imani na kufanyika biashara kwa maeneo mapya ya baadae.
Na hayo ndiyo yamekuwa mawazo yangu na ushauri wangu kwenye vikao vyote tulivyokaa lakini yakapuuzwa.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akiagana na wananchi mmoja mmoja walioweza kumfikia mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kata ya Igoma Wilaya ya Nyamagana lengo likiwa ni kumshukuru Rais Dk John Magufuli kuwarejesha wamachinga kufanya shughuli zao maeneo ya Mjini. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.