Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na wananchi mara baada ya kuingia wilayani Ukerewe. PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG. |
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoa wa Mwanza Injinia Athony Sanga akitoa ufafanuzi wa mradi wa maji wilaya ya Ukerewe mbele ya Makamu wa Rais Serikali awamu ya 5. |
Ukerewe. Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa mji wa Nansio katika wilaya ya Ukerewe mkoani hapa kuepuka ujenzi wa nyumba ambazo hazina huduma za vyoo vya ndani.
Lengo la agizo hilo ni pamoja na kupunguza kiwango cha uchafuzi wa maji ya ziwa,kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi kuchimba vyoo vya shimo ambavyo alisema mara nyingi miundombinu yake siyo rafiki kwa usafi wa mazingira,hasa kandokando ya ziwa.
MamaSamia alitoa agizo hilo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji huo kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa majiisafi na usafi wa mazingira ziwa Victoria awamu ya pili ambao umetekelezwa kwa gharama ya sh10.9 bilioni.
Makamu huyo wa Rais ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mradi huo ambao umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika,kupitia nchi wanachama wsa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Licha ya kutumia muda mwingi wa hotuba yake kujibu mabango ya wananchi,Makamu wa Rais pia aliiagiza Wizara ya maji na umwagiliaji kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Jijini Mwanza kushirkiana na wakazi wa mji huo kulinda miundombinu ya mradi.
Akisoma taarifa mbele ya Makamu sa Rais,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Emmanuel Kalobelo alisema mradi utawanufaisha wakazi zaidi ya 80,000 wa mji wa Nansio pamoja na vijiji vya Nantare, Kakerege, Hamkoko, Bukongo, Nkilizya, Kagera, Nakatunguru, Malegea na Bulamba.
Alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi mingine miwili inayotekelezwa kitaifa katika miji ya Sengerema na Geita mkoani.
Kwa upande wake,mwakilishi wa Kamisheni ya Bonde la ziwa Victoria,Dk Matano aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukamilisha mradi huo kwa wakati, na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na miradi mingine 12 inayotekelezwa katika nchi nyingine tano ambazo ni wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais juzi alihitimisha ziara ya siku tatu mkoani Mwanza ambapo alitembelea na kuweka mawe ya misingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Sengerema, Misungwi, Kwimba na Magu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.