Wachambuzi wa Soka toka kituo cha Redio Jembe Fm ya jijini Mwanza wamelipambanua suala hilo na kulichimba kwa undani kisha kuja na majibu kuwa hoja hiyo haitekelezeki, na ni hoja ya kuliondoa soka la Tanzania kwenye ramani ya soka Ulimwenguni.
Simba wametamka bayana kuwa wapo tayari kulipa gharama za waamuzi hao kuanzia mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili ili haki itendeke kwakua watani wao wamekuwa wakipendelewa mara kwa mara na marefarii wa hapa nchini.
Msimamo huo umetolewa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari klabuni hapo na kusema kuwa kwasasa hawatakuwa tayari kuona haki zao zikidhulumiwa kwa namna yoyote na wataanzia mzunguko wa pili unaotarajia kuanza Disemba 17.
Fuatilia kilichojiri ndani ya uchanbuzi katika kipindi cha KIPENGA kinachoruka kila jumamosi saa 07:00 asubuhi hadi 10:00 asubuhi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment