Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Mbogo Mining Wilayani Magu ili kupunguza changamoto ya madawati mashuleni. |
NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza
MKUU wa wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza Khadija Nyembo, amewaomba wawekezaji kuwekeza na kutoa misaada katika sekta ya elimu ili kupunguza Changamoto zinazo ikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na upungufu wa madarasa katika baadhi ya shule.
Wito huo umekuja baada ya wilaya hiyo kuwa na uhitaji wa madara 1340 huku yaliyopo yakiwa 935 hali ambayo inayonesha kuwepo kwa wanafunzi kukosa vyumba vya kusomea.
Hayo ameyasema juzi wakati akipokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milion 3, kutoka Kampuni ya uagizaji na usambazaji wa Baruti nchini (Mbogo Mining) ambapo amesema kuwa kuwekeza katika elimu ni sadaka ambayo itasaidia vizazi na vizazi kwa miaka ijayo.
“Ukifanya suala zuri katika elimu ni sadaka tosha, na Suala la madawati tunalijua lilivyo tete katika maeneo mengi, katika wilaya yangu nimekamilisha lakini shida ipo upande wa madarasa kwani idadi ya wanafunzi ni kubwa ikilinganishwa na madarasa yaliyopo”amesema Nyembo.
“Kampuni imeanza mahusiano mazuri na jamii inayo tuzunguka hususani katika eneo la Uwekezaji, tangu mwaka 2014 tulipo anza kazi tulikuwa tukijihusisha na shughuli za maendeleo kwa wananchi wa kijiji cha Ihayabuyaga na wilaya kwa nzima ”ameeleza Edward.
Aliitaja baadhi ya misaada waliyoitoa kuwa ni pamoja na Ujenzi wa vyumba viwili katika shule za msingi za Ilendeja na Bukandwe, ukarabati wa choo cha walimu katika shule ya msingi Ilendeja, Mifuko 100 ya Saruji katika ofisi ya mkuu wa wilaya Magu na mbao za shilingi Laki 6.
Misaada mingine iliyotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na ujenzi wa geti katika kituo cha Polisi Kisesa na Kiti cha mkuu wa kituo hicho na madawati 50 waliyokabidhi, tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo, imeweza kuchangia jamii kiasi cha sh. Milion 99.7katika mwaka wa fedha 2014\2015.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.