Akizungumza katika kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto Balozi wa Ireland nchini Tanzania Paul Sherlock ametoa wito huo kwa serikali wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kupewa fursa ya kurejea masomoni.
Balozi wa Ireland Nchini Tanzania PAUL SHERLOCK amewasili mkoani Mwanza akitokea jijini Dar es salaam, kushiriki katika kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia ambapo ametembelea Dawati la jinsia ktk makao makuu ya polisi mkoani mwz na kuelezwa mafanikio yaliopatikana tangu kuanzishwa kwake.
MISUNGWI.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini misungwi balozi huyo wa Ireland nchini ameishauri serikali kufikiria upya suala la wanafunzi wanaokatishwa ndoto zao kutokana na mimba za utotoni, kupewa fursa ya kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Aidha Balozi wa Ireland Nchini PAUL SHERLOCK amemtembelea mjane NURU KHALID mkazi wa kijiji cha usagara wilayani misungwi ambaye amerejeshewa mali zake zenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 50 alizokuwa amedhulumiwa na ndugu wa mumewe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake la kivulini YASINI ALLY analia na mwamko mdogo kwa jamii katika kanda ya ziwa kuwapa elimu watoto wa kike.
Shirika lisilo la kiserikali la Kivulini limezindua kampeni ya siku kumi na sita ya kupinga ukatili wa kijinsia ambapo limekuwa likihamasisha wananchi, mashirika ya dini, serikali na wadau mbalimbali kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment