ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 16, 2016

MUDA WA VITAMBULISHO VYA TAIFA WAFANYAKAZI WA UMMA MWANZA WAONGEZWA.

Serikali imetangaza kuongeza muda wa usajili wa vitambulisho vya taifa kwa wafanyakazi wa umma nchini baada ya kubaini kuwa muda wa siku 14 zinazoishia jumatatu hautoshelezi kuandikisha wafanyakazi wote wanaofikia zaidi ya laki tano na nusu nchini.

Nyogeza hiyo ya muda imetolewa mkoani mwanza na Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora ANGELA KAIRUKI ambaye ameitaka mamlaka ya vitambulisho vya taifa(NIDA)kuhakikisha kuwa inaandikisha wafanyakazi wote wa umma wakiwemo wenye vyeti na wasio na vyeti vya kitaalumu.


Ziara ya waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora ANGELA KAIRUKI inayomwezesha kujionea namna zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa kwa wafanyakazi wa umma linavyoendelea mkoani mwanza.


Kituo chake cha kwanza kilikuwa wilayani misungwi.


-ELIUD MWAITELEKE- mkurugenzi wa halmashauri  ya wilaya hiyo ELIUD MWAITELEKE.
Changamoto zinazokabili zoezi hilo linalotekelezwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa(NIDA)zikabanishwa na baadhi ya wafanyakazi wa misungwi.


Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala bora ANGELA KAIRUKI amehitimisha ziara yake kwa kukutana na viongozi wa mkoa wa mwanza pamoja na  wakuu wa idara za halmashauri za misungwi,ilemela na jiji la Mwanza.

- DAUD ABDALAH-AFISA MSAJILI NIDA MWANZA.


- Angela Kairuki - Waziri wa Nchi Utumishi na Utawala Bora.
Aidha  amewaondoa hofu wafanyakazi kuhusu zoezi hilo.




Kisha msafara wa waziri KAIRUKI ukaelekea katika wilaya za ilemela na nyamagana ambapo amewataka maafisa utumishi kuongeza uwajibikaji ili kutatua kero za wafanyakazi.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.