KAYA 25 wilayani Nyamagana jijini hapa zimenufaika na mradi wa uimarishaji wa kaya masikini unaotolewa na shirika lisilo la kiserikali la SOS Children’s Tanzania kwa kupatiwa elimu ya ujasiliamali na uwezeshwaji wa kifedha kutokana na ugumu wa maisha uliokuwa unawakabili.
Wakiongea na mtandao huu baadhi ya wanufaika na mradi huo walisema kuwa wanashukuru shirika hilo kuwasaidia kutoka kwenye hali mbaya ya kimaisha na kwamba hali waliokuwa nayo hata kupata milo mitatu kwa siku ili kuwa ni shida kwao.
“Kiukweli maisha ya awali yalikuwa magumu sana maana tulikuwa tunakula uji tu na watoto walikuwa hawasomi kutokana na kukosa mahitaji ya shule hiyo lakini toka tauingie kwenye mradi huu uhakika wa milo mitatu ni ya huakika na kwa sasa watoto wetu wanalipiwa ada ya shule pamoja na vifaa vya shule”, walisema
Mmmoja wa wanufaika hao Chacha Mkami ni mkazi wa Bugarika jijini hapa alisema awali alikuwa anapanga chumba huku akiwa na watoto saba lakini kwa uwezeshwaji aliopata kutoka kwa SOS amejenga nyumba yake huku akiendelea na biashara yake.
Kwa upande wake Tatu Abduh alisema kuwa anashukuru kukutana na shirika hili ambalo limebadilisha maisha yake baada ya kumpatia elimu ya kucheza hisa pamoja na kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuliomba shirika hilo licha ya kuamua kuachana nao lakini waendele kuwakumbuka kwa kuendelea kwasaidia pale itakapo bidi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Elizabeti Swai alisema kuwa kaya hizo walianza kuzisaidia toka mwaka 2010 na sasa wamaeamua kuwahitimisha kwa kuanza kutafuta kaya nyingie masikini kwa kuwa bado wahitaji ni wengi.
“Kwenye mradi huu hadi sasa tuna wanafunzi 1200 ambao tunaendelea kuwasaidia mahitaji ya shule kama viatu sare za shule na madaftari huku tukitarajia kuanza na kaya nyingine amabo tutaziingza kwenye mradi huu”, alisema Elizabeti.
Shirika la SOS mbali na kusaidia kuimarisha kaya masikini pia wanajishughulisha na utoaji malezi mbadala kwa watoto yatima waliopoteza wazazi wao ikiwa na kutelekezwa baada ya kuzaliwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.