Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Mwandamizi Ahamed Msangi amedhibitisha kutokea wa kitukio hilo cha ubakaji na kwamba mtuhumiwa amekamatwa na tayari jalada lake la mashitaka limepelekwa kwa mwanasheria wa serikali, hivyo muda wowote kuanzia hivi sasa atafikishwa mahakamani, ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Inasemekana kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu alikuwa na kawaida (tabia) ya kumbaka binti yake kwa muda mrefu, kabla ya ndugu kumfumania na kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na taarifa polisi kuhusiana na kitendo hicho.
Msangi ameeleza kuwa baadae binti aliweza kupelekwa hospitali ya kwa ajili ya uchunguzi ndipo ikathibitika kwamba ni kweli amebakwa.
Kwa mjibu wa mtoto aliyekuwa akitendewa kitendo hicho amesema kuwa toka baba yake mzazi alipotengana na mama yake mzazi amekuwa akimfanyia kiitendo hicho kwa kumlaza kila alipokuwa akitegeshea watu wote hawapo nyumbani hapo.
Ameeleza kuwa kutokana na kitendo hicho kutomfurahisha aliwahi kumwambia bibi yake kile anachofanyiwa lakini bibi yake alikataa kumwamini kabla ya ndugu ambao ni kaka zake kumkuta baba huyo akimbaka na kuwa chanzo cha kugundurika uovu huo.
Kwa upande wake Erick Karongo afisa uelimishaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la foundation Karibu Tanzania (FKT) ambalo linajishughulisha na kupinga ukatili wa kijinsia limeaasa wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao ili kuwakinga na ukatili ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.